Cv YA Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025
Klabu ya Yanga SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili mlinzi mahiri, Boka Chadrak, kutoka FC Saint Eloi Lupopo ya Kinshasa, Congo. Boka, ambaye ni mlinzi wa kushoto, anasifika kwa uwezo wake wa kushambulia na kujilinda kwa haraka, na atakuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu ya Wananchi Yanga sc kwa msimu wa 2024/2025.
Cv YA Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025
Maelezo | Taarifa |
Jina la Kuzaliwa | Chadrack Issaka Boka |
Tarehe ya Kuzaliwa/Umri | Nov 20, 1999 (24) |
Mahali pa Kuzaliwa | Kinshasa, DR Congo |
Uraia | DR Congo |
Nafasi | Beki – Kushoto |
Mguu wa Kutumia | Kushoto |
Klabu ya Sasa | Yanga SC |
Amejiunga Tarehe | 8-Jul-24 |
Ametoka Klabu | FC Saint Eloi Lupopo |
Uwezo na Ujuzi wa Boka Chadrak
Boka Chadrak ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha kupandisha mashambulizi na kushuka haraka. Uwezo wake wa kuoverlap, yaani kupanda mbele kushambulia na kurudi haraka kujilinda, unamfanya kuwa chaguo bora kwa kocha Miguel Gamondi ambaye ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1. Mfumo huu unahitaji mabeki wenye uwezo wa kushambulia na kujilinda kwa kasi, kitu ambacho Boka anafanya kwa ufanisi mkubwa kutokana pumzi pamoja na spidi alionayo.
Mfumo wa 4-2-3-1 na Nafasi ya Boka Chadrak
Kocha Miguel Gamondi ametumia sana mfumo wa 4-2-3-1 katika msimu uliopita, na mara nyingi mfumo huu umekuwa ukitumika na timu zinazofanya pressing kwa kasi kama Yanga SC. Ingizo la Boka Chadrak linaongeza ufanisi wa mfumo huu kutokana na uwezo wake wa kuchezeshwa kama invited winger, ambapo atapanua uwanja na kuingia ndani kwa ajili ya kupiga pasi za hatari au krosi.
Katika mfumo huu, viungo washambuliaji watatu wanaocheza nyuma ya mshambuliaji wanategemea zaidi mabeki wa pembeni kama Boka na Kouasi Yao kupanua uwanja. Hii inafanya Boka kuwa na jukumu muhimu katika kuandaa mashambulizi na kutoa msaada kwa washambuliaji.
Mapendekezo ya Mhariri;
- Hii apa CV ya Omary Abdallah Kiungo Mpya Wa Simba 2024/2025
- CV ya Fadlu Davids: Kocha Mpya wa Simba SC (2024/2025)
- Cv ya Valentino Mashaka Mshambuliaji Mpya wa Simba Sc 2024
- CV Ya Abdulrazak Hamza Beki Mpya Wa Simba 2024/2025
- CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
- Cv Ya Steven Mukwala Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
- Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
- Majina ya Wachezaji Wapya Simba 2024/2025
Weka Komenti