Cv ya Dimitar Pantev Kocha Mpya wa Simba Sc 2025

Cv ya Dimitar Pantev Kocha Mpya wa Simba Sc 2025

Klabu ya Simba SC imethibitisha rasmi kumteua Dimitar Pantev kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo kwa msimu wa 2025, akichukua mikoba iliyoachwa wazi na Fadlu Davids aliyetimkia Raja Casablanca ya Morocco.

Pantev, raia wa Bulgaria mwenye umri wa miaka 49, anakuja nchini akiwa na rekodi ya mafanikio barani Afrika baada ya kuinoa klabu kadhaa na kushinda mataji ya ligi katika mataifa mawili tofauti.

Kocha huyu aliyetambulika kwa falsafa yake ya soka la kushambulia, amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba SC, klabu inayolenga kurejea kwenye utawala wa soka la Tanzania na pia kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ya CAF.

Wasifu wa Dimitar Pantev

  • Jina kamili: Dimitar Pantev
  • Umri: Miaka 49
  • Tarehe ya kuzaliwa: 26 Juni 1976
  • Mahali: Varna, Bulgaria
  • Uraia: Bulgaria
  • Leseni: Leseni ya UEFA Pro (ngazi ya juu ya ukocha barani Ulaya)

Cv ya Dimitar Pantev Kocha Mpya wa Simba Sc 2025

Safari ya Dimitar Pantev Kama Kocha

Dimitar alianza kazi yake ya ukocha katika kikosi cha vijana cha Varna City. Baada ya hapo, alijiunga na klabu ya Al Ahli Hebron kama Kocha Msaidizi kabla ya kupata nafasi ya kuongoza vikosi vya wakubwa kama Flamengo, Victoria United, Johansen, Orapa, na hatimaye Gaborone United.

Dimitar Pantev ameonyesha ujuzi mkubwa katika kazi yake ya ukocha hususan barani Afrika. Kabla ya kutua Simba SC, ameifundisha jumla ya klabu tano barani humo. Safari yake imeanzia Victoria United (Cameroon) ambako alikiongoza kikosi hicho kubeba ubingwa wa kwanza katika historia ya klabu hiyo. Baada ya hapo alihamia FC Johansen (Sierra Leone), kisha Orapa United na Gaborone United zote za Botswana.

Akiwa na Gaborone United, alifanikiwa kuipa klabu hiyo ubingwa wa 8 wa Ligi Kuu ya Botswana, jambo lililomfanya kujiimarisha zaidi kama kocha mwenye rekodi ya mafanikio. Kwa kipindi cha miaka mitano barani Afrika, amebeba mataji mawili ya Ligi Kuu katika mataifa mawili tofauti, ikiwemo Cameroon na Botswana.

Mbali na soka la kawaida, Pantev pia ana historia kubwa katika mchezo wa Futsal. Akiwa kocha, ameiongoza timu yake kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu ya Bulgaria ya Futsal, jambo linaloonyesha upeo wake mpana wa kiufundi katika michezo tofauti.

Historia ya Dimitar Pantev Akiwa Kama Mchezaji

Kabla ya kuwa kocha, Dimitar Pantev aliwahi kucheza soka kwenye nafasi ya kiungo. Alicheza katika ngazi ya Ligi Kuu nchini Bulgaria, akipita katika timu kadhaa ikiwemo:

  • Cherno More
  • FC Suvolovo
  • Chernomorets Byala
  • Kaliakra Kavarna
  • Chernomorets Balchik
  • Volov Shumen
  • Dobrudzha
  • Vladislav
  • Shabla
  • Spartak Varba

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Singida BS Yaendeleza Ubabe Mbele ya Mashujaa na Kubaki Kinara wa Ligi Kuu Bara
  2. Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  3. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  4. Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
  5. Arsenal yapata ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Newcastle United
  6. Wapinzani wa Simba Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika CAF
  7. Azam FC Yafuzu Raundi ya Pili CAFCC Baada ya Ushindi wa 4-0 Dhidi ya El Merriekh
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo