CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026

CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026

Timu ya wananchi Yanga SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa msimu mpya wa 2025/2026, ambapo leo hii imemtambulisha rasmi kiungo mchezeshaji kutoka Ivory Coast, Mohamed Doumbia (26), kuwa sehemu ya safu yao ya kati. Usajili huu unaongeza nguvu mpya katika kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara, huku ukiongeza ushindani mkubwa ndani ya timu.

CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026

Wasifu wa Mohamed Doumbia

Mohamed Doumbia alizaliwa tarehe 25 Desemba, 1998 katika jiji la Abidjan, Ivory Coast. Kiungo huyu mwenye urefu wa 1.74 mita hutumia mguu wa kulia kama mguu wake wa msingi uwanjani. Ana uraia wa Ivory Coast na anacheza katika nafasi ya Kiungo wa Kati.

Kwa takribani muongo mmoja, Doumbia ameonesha uwezo mkubwa katika safu ya kiungo, akicheza katika ligi mbalimbali barani Ulaya na Afrika, na sasa anatarajiwa kuleta uzoefu huo mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu ujao.

Historia ya Uhamisho wa Mohamed Doumbia

CV ya Mohamed Doumbia kiungo mpya wa Yanga 2025/2026 inaonesha mchezaji mwenye uzoefu mpana katika soka la kimataifa, akiwa amepitia vilabu kadhaa vya ushindani:

Msimu Tarehe ya Uhamisho Aliyetoka Aliyejiunga Thamani ya Soko Ada ya Uhamisho
2024/2025 17 Machi 2025 SC Majestic Bila Klabu €350k Bure
2024/2025 28 Januari 2025 Bila Klabu SC Majestic €350k Bure
2024/2025 01 Julai 2024 Slovan Liberec Bila Klabu €400k Bure
2021/2022 17 Februari 2022 Dukla Prague Slovan Liberec €150k Uhamisho Huru
2017/2018 01 Januari 2018 Ekenäs IF Dukla Prague €50k €50k
2016/2017 01 Januari 2017 Haijulikani Ekenäs IF Haijatajwa Uhamisho Huru

Kwa mujibu wa historia yake, Doumbia amewahi kuitumikia vilabu vya SC Majestic (Burkina Faso), Slovan Liberec na Dukla Prague (vyote vya Jamhuri ya Czech), pamoja na Ekenäs IF ya Finland. Safari yake ya soka inaonesha mchezaji mwenye uthabiti wa kiufundi, aliyezoea kushindana katika mazingira tofauti ya ligi mbalimbali.

Safari Yake ya Kitaaluma

  • 2017-2018: Doumbia alianza safari yake ya kimataifa barani Ulaya alipokuwa Ekenäs IF nchini Finland.
  • 2018-2022: Baada ya Finland, aliingia katika soka la Jamhuri ya Czech akijiunga na Dukla Prague ambapo alidumu kwa takribani miaka minne kabla ya kuhamia Slovan Liberec.
  • 2024-2025: Alirejea barani Afrika na kujiunga na SC Majestic ya Burkina Faso kabla ya kuachana na klabu hiyo Machi 2025.
  • 2025: Hatimaye, amejiunga rasmi na Yanga SC kama mchezaji huru.

Sehemu ya Usajili Mpya Yanga SC 2025/2026

Mohamed Doumbia anakuwa mchezaji wa nane mpya kusajiliwa na Yanga SC kwa msimu wa 2025/2026, na mchezaji wa tano wa kigeni katika kikosi hicho. Wengine waliotangulia ni:

  1. Lassine Kouma – Kiungo kutoka Stade Malien, Mali
  2. Balla Mousa Conte – Kiungo kutoka CS Sfaxien, Tunisia
  3. Andy Bobwa Boyeli (24) – Mshambuliaji kutoka Sekhukhune United FC, Afrika Kusini
  4. Ange Celestin Ecua – Mshambuliaji kutoka Zoman FC, Ivory Coast

Kwa upande wa wazawa, Yanga pia imesajili wachezaji wafuatao:

  1. Abdulnasir Mohamed Abdallah – Kiungo kutoka Mlandege, Zanzibar
  2. Nizar Abubakar Othman ‘Ninju’ – Kiungo kutoka JKU, Zanzibar
  3. Offen Francis Chikola – Winga kutoka Tabora United

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Cv ya Mohammed Bajaber Kiungo Mshambuliaji Mpya Simba Sc 2025/2026
  2. Picha za Wachezaji Wapya wa Simba 2025/2026
  3. Pamba Jiji FC Yamtambulisha Francis Baraza Kama Kocha Mkuu 2025/2026
  4. CV ya Alassane Kante Kiungo Mpya Simba 2025/2026
  5. CV Ya Rushine De Reuck Beki Mpya wa Simba 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo