Droo ya Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
Droo ya michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa msimu wa 2025/2026, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, imefanyika rasmi, na matokeo yake yamewaweka wawakilishi wa Tanzania Yanga SC, Simba SC, Azam FC na Singida Black Stars kuanzia hatua ya awali wakiwa ugenini. Droo hiyo ilipangwa katika Studio za Azam Media, Dar es Salaam, na imeashiria rasmi mwanzo wa safari ya vilabu 58 kutoka bara zima kuelekea hatua ya makundi na hatimaye taji la heshima la klabu Afrika.
Ratiba Rasmi ya Hatua za Awali
Kwa mujibu wa CAF, hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho 2025/2026 itaanza kati ya 19–21 Septemba 2025 kwa mechi za kwanza, ikifuatiwa na mechi za marudiano kati ya 26–28 Septemba 2025. Timu zitakazofaulu zitatinga raundi ya pili ya awali, itakayochezwa kati ya 17–19 Oktoba 2025 (mechi ya kwanza) na 24–26 Oktoba 2025 (mechi ya marudiano). Mshindi wa raundi hiyo atafuzu hatua ya makundi itakayoanza 21 Novemba 2025, kabla ya kuingia hatua ya mtoano mnamo 13 Machi 2026.
Mechi za Wawakilishi wa Tanzania Katika Michuano ya CAF
- Yanga SC – Mabingwa wa Ligi Kuu Bara watakabiliana na Wiliete Benguela ya Angola katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakiwa na lengo la kwenda mbali zaidi baada ya msimu uliopita kuishia hatua ya makundi.
- Simba SC – Watani wa jadi wa Yanga na washiriki wa msimu uliopita wa Kombe la Shirikisho, ambapo walifika fainali, watakutana na Gaborone United ya Botswana.
- Azam FC – Wawakilishi wa Kombe la Shirikisho watakutana na EL Mereikh ya Sudan. Azam, ambayo msimu uliopita iliishia hatua ya awali, sasa iko chini ya Kocha Florent Ibenge na inalenga kufuata nyayo za Namungo FC, waliowahi kufika hatua ya makundi.
- Singida Black Stars – Kwa mara ya kwanza kushiriki michuano ya kimataifa, Singida itakabiliana na Rayon Sports ya Rwanda, inayonolewa na Robertinho Oliveira, aliyewahi kuifundisha Simba. Timu hii imepigiwa upatu kutokana na uwekezaji mkubwa na uzoefu wa Kocha Miguel Gamondi.
Droo ya Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
Jumla ya vilabu 58 vitashiriki katika Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026, ambapo baadhi ya vigogo wa soka barani wamepewa nafasi ya moja kwa moja kuanzia raundi ya pili kutokana na alama zao za CAF Club Ranking. Miongoni mwao ni Wydad AC (Morocco), USM Alger (Algeria), CR Belouizdad (Algeria), Zamalek SC (Misri), Al Masry SC (Misri) na Stellenbosch FC (Afrika Kusini).
Timu Ya Kwanza | Timu Ya Pili |
Asante Kotoko | Kwara Utd |
Génération Foot | Amadou Diallo |
Bhantal Fc | Hafia Sc |
Usfa | As Gbohloe-Su |
Abia Warriors | Djoliba Ac |
Asn Nigelec | Ocs |
Stade Tunisien | Asc Snim |
Aigle Royal | Fc San Pedro |
Black Man Warrior | Coton Sport |
Dekadaha Fc | Alzamala Umr |
Wolitta Dicha Sc | Libya 2 |
Nec Fc | Nairobi Utd. Fc |
Al Ahli Madani | Ess |
As Port | Kmkm Sc |
El Merriekh Bentiu | Azam Fc |
Flambeau Du Centre | Libya 1 |
Rayon Sport Fc | Singida Black Stars |
Foresters Fc | Fc 15 Agosto |
Fc 105 | Zesco Utd |
M. Wanderers | Jwaneng Galaxy |
Rd Congo 2 | Djabal Fc |
Kabuscorp De P | Kaizer Chiefs |
Rd Congo 1 | Pamplemousses |
Young Africans Fc | Royal Leopards |
F. De Maputo | As Fanalamanga |
Cd 1 Agosto | As Otohô |
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mshahara wa Celestin Ecua Yanga 2025/2026
- Msimamo Kundi la Tanzania CHAN 2024
- Mohamed Hussein Shabalala Ajiunga na Yanga SC Baada ya Miaka 11 Simba
- Ratiba ya CHAN 2025 Mechi za Makundi
- Orodha ya Wachezaji Wazawa Yanga Sc 2025/2026
- CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026
- Cv ya Mohammed Bajaber Kiungo Mshambuliaji Mpya Simba Sc 2025/2026
Leave a Reply