Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025/2026
Droo ya robo fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika imefanyika rasmi leo mjini 6th of October City, nchini Misri, na kuweka wazi ramani kamili ya safari ya kila klabu kuelekea fainali ya mashindano hayo ya msimu wa 2025/2026.
Sherehe ya upangaji ratiba hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Shirikisho la Soka la Misri baada ya kukamilika kwa hatua ya makundi Jumapili iliyopita, ambapo timu nane zilifanikiwa kufuzu hatua ya mtoano.
Timu Zilizofuzu Robo Fainali
Baada ya kukamilika kwa hatua ya makundi, klabu nane zilijihakikishia nafasi katika robo fainali ya mashindano:
- Al Masry (Misri)
- CR Belouizdad (Algeria)
- Olympique Safi (Morocco)
- Wydad Athletic Club (Morocco)
- Otoho (Congo)
- Zamalek (Misri)
- Maniema Union (DR Congo)
- USM Alger (Algeria)
Ratiba ya Mechi za Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF
Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025/2026 imepanga michezo ifuatayo:
- QF1: Al Masry (Misri) vs CR Belouizdad (Algeria)
- QF2: Olympique Safi (Morocco) vs Wydad Athletic Club (Morocco)
- QF3: Otoho (Congo) vs Zamalek (Misri)
- QF4: Maniema Union (DR Congo) vs USM Alger (Algeria)
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Machi 15
Marudiano yatapigwa Machi 22
Njia ya Nusu Fainali
Mbali na kupanga robo fainali, droo pia imeonyesha mwelekeo wa hatua ya nusu fainali:
- Mshindi wa QF4 vs Mshindi wa QF2
- Mshindi wa QF1 vs Mshindi wa QF3
Mpangilio huu unaweka wazi safari ya kuelekea ubingwa huku kila timu ikijua mapema mpinzani anayemsubiri endapo itafanikiwa kusonga mbele.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply