Fei Toto na Aziz KI: Kinyanganyiro cha Mfungaji Bora Ligi Kuu Kushika Moto
- Nyota wa Azam Fei Toto Afikisha Mabao 15 Ligi Kuu ya NBC Tnzania, Sasa Amemkuta Aziz KI Kwenye Kinyang’anyiro cha Kiatu cha Mfungaji Bora msimu wa 2023/2024.
Fei Toto na Aziz KI: Kinyanganyiro cha Mfungaji Bora Ligi Kuu Kushika Moto
Vita vya kuwania kiatu cha dhahabu katika Ligi Kuu Tanzania vinazidi kupamba moto. Nyota wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ alifunga bao muhimu katika mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar, bao lililomfikisha kufikisha jumla ya mabao 15 msimu huu. Idadi hii inamuweka sambamba na mshambuliaji hatari wa Yanga, Stephane Aziz KI, katika kinyang’anyiro hiki cha kusisimua.
Azam ilishinda mchezo huo wa jana kwa mabao 2-0, huku bao la pili likifungwa na Gibril Sillah. Ushindi huu unaifanya Azam kudumisha nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 57, wakifuata nyuma vinara Yanga wenye pointi 65. Matokeo haya yanaendelea kuiweka Mtibwa Sugar kwenye nafasi mbaya ya kushuka daraja, kwani huu ni mshindo wao wa 16 katika michezo 25 waliyocheza hadi sasa.
Katika historia ya hivi karibuni ya mechi baina ya Azam FC na Mtibwa Sugar, Azam imetawala. Rekodi zinaonyesha ushindi wa Azam wa mabao 5-0 katika mzunguko wa kwanza, na ushindi mwengine wa mabao 4-3 kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Morogoro.
Akizungumzia matokeo ya mchezo wa jana, kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila, alikiri timu yake ilipambana lakini makosa madogo ya kibinafsi yaliwagharimu. Alionesha matumaini ya mapambano katika michezo ijayo ili kuinusuru timu yake. Kocha wa Azam, Youssouph Dabo, alipongeza viwango walivyoonyesha wachezaji wake, ingawa mvua za kipindi cha pili zilipunguza kasi ya mchezo.
Weka Komenti