Hizi Apa Picha za Jezi mpya za Simba 2025/2026
Klabu ya Simba SC hatimaye imezindua rasmi jezi zake mpya kwa ajili ya msimu wa mashindano wa 2025/26, zitakazotumika kwenye michezo ya nyumbani, ugenini pamoja na jezi ya tatu (third kit). Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, ambapo mashabiki na wanachama wa klabu hiyo walijitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria lililopambwa na shamrashamra na burudani za aina yake.
Jezi Mpya za Simba 2025/2026 Zazinduliwa kwa Hadhira Kubwa
Katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, alisisitiza kuwa jezi mpya za msimu wa 2025/2026 ni za ubora wa hali ya juu na zimezingatia hadhi ya klabu pamoja na matakwa ya mashabiki.
Mangungu alieleza kuwa tangu mwanzo wa mchakato wa kupata muundo wa jezi hizo, klabu iliahidi kusaini mkataba na mkandarasi wa chapa ya kimataifa, jambo ambalo sasa limekamilika kupitia ubia na kampuni ya Jayrutty. Alisisitiza pia kuwa heshima ya jezi na chapa ya Simba si jukumu la viongozi pekee bali ni jukumu la kila shabiki na mwanachama wa klabu hiyo:
“Jukumu la kuilinda chapa ya Simba sio la Mwenyekiti wa Klabu au Bodi pekee, bali ni jukumu la Wanasimba wote. Tunaamini kabisa bidhaa tunazozitoa zitakuwa za kiwango cha kimataifa,” alisema Mangungu.
Hizi Apa Picha za Jezi mpya za Simba 2025/2026
Mapendekezo ya Mhariri:
- Tarehe za Mechi za Simba VS Yanga 2025/2026: Ratiba ya Dabi ya Kariakoo
- Yanga Kutumia Benjamin Mkapa Kama Dimba la Nyumbani Huku Simba Kuhamia KMC Complex
- Msimamo wa Ligi Kuu England EPL 2025/2026
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026
- Simba SC Kufanya Maamuzi Magumu Kuhusu Hatma ya Kipa Wao
- Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2025
- Mechi ya Pili ya Dabi ya Kariakoo Simba vs Yanga Kuchezwa Desemba 13 2025
Leave a Reply