Jeshi la Zimamoto Latangaza Nafasi Mpya za Ajira kwa Vijana, Fahamu Sifa na Jinsi ya Kuomba

Jeshi la Zimamoto Latangaza Nafasi Mpya za Ajira kwa Vijana, Fahamu Sifa na Jinsi ya Kuomba

Dodoma. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetangaza nafasi mpya za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia kidato cha nne, kidato cha sita na shahada katika fani mbalimbali, kwa ajili ya ajira ngazi ya Konstebo.

Tangazo hilo limetolewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo kwa mujibu wa kifungu cha 14(4) cha Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427 pamoja na Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Utumishi za mwaka 2008.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wanatakiwa kuzingatia masharti yote yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na uadilifu, uwezo wa kifedha na kimwili, pamoja na utayari wa kuhudhuria mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji mara baada ya kuchaguliwa. Jeshi limeeleza kuwa maombi yote yatawasilishwa kupitia mfumo rasmi wa ajira wa Jeshi hilo.

Sifa za Waombaji – Kidato cha Nne

Waombaji wa ngazi hii wanapaswa kuwa:

  • Raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

  • Na Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.

  • Na afya njema kimwili na kiakili.

  • Wasio na kumbukumbu za uhalifu.

  • Hawajaoa au kuolewa.

  • Wasio na alama za michoro mwilini (tattoos).

  • Hawajawahi kutumia dawa za kulevya.

  • Tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji.

  • Hawajawahi kuajiriwa serikalini.

  • Wenye urefu usiopungua futi 5.7 kwa wanaume na 5.4 kwa wanawake.

  • Tayari kushiriki hatua zote za usaili watakapoitwa.

  • Tayari kufanya kazi popote watakapopangiwa baada ya mafunzo.

  • Na umri kati ya miaka 18 hadi 25.

Jeshi la Zimamoto Latangaza Nafasi Mpya za Ajira kwa Vijana, Fahamu Sifa na Jinsi ya Kuomba

Taaluma Ngazi ya Kidato cha Nne au Sita

Jeshi limeainisha nafasi kwa vijana wenye ujuzi wa kitaaluma katika maeneo yafuatayo:

  • Madereva wa magari makubwa

  • Wauguzi ngazi ya Stashahada

  • Taaluma za Zimamoto na Uokoaji

  • Matabibu ngazi ya Stashahada

  • Fundi mchundo wa magari

  • Wazamiaji na waogeleaji

  • Wanamichezo

  • Brass band

  • Waandishi wa habari na waendesha ofisi

  • TEHAMA ngazi ya Stashahada

  • Mafundi umeme wa ndege ngazi ya Stashahada

Masharti ya Waombaji – Taaluma Kidato cha 4/6

Waombaji wanapaswa kuwa:

  • Na sifa zote za msingi zilizoorodheshwa kwa ngazi ya kidato cha nne.

  • Na umri kati ya miaka 18 hadi 28.

  • Kwa wazamiaji na waogeleaji, uthibitisho wa vitendo utafanyika wakati wa usaili.

  • Kwa madereva, ni lazima kuwa na leseni daraja E na watapimwa kwa vitendo wakati wa usaili.

Ngazi ya Shahada

Kwa ngazi ya shahada, nafasi zimetolewa kwa vijana waliosomea fani zifuatazo:

  • Uhandisi Bahari

  • TEHAMA

  • Uhandisi wa Ndege

  • Wakadiriaji Majenzi (QS)

  • Sheria (waliohitimu mafunzo ya vitendo katika shule ya sheria)

  • Mafundi wa gesi

  • Uhandisi wa ujenzi

  • Uhandisi mitambo

  • Uhandisi umeme

Masharti ya Waombaji – Shahada

Waombaji wanapaswa kuwa na:

  • Sifa zote za msingi zilizoainishwa kwa kundi la kwanza.

  • Umri kati ya miaka 18 hadi 28.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kiunganishi:

👉 https://ajira.zimamoto.go.tz

Mwisho wa kupokea maombi ni Desemba 03, 2025.

Nyaraka Zinazotakiwa Kuambatanishwa

Waombaji wanapaswa kuwasilisha:

a) Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono, ikielekezwa kwa:
Kamishna Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
1 Mtaa wa Zimamoto,
S.L.P 1509,
41102 Dodoma.

b) Fomu ya uthibitisho wa afya njema iliyosainiwa na mganga wa serikali.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  2. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE)
  3. Kidato cha Nne Kuanza Mitihani ya Taifa Kesho November 17 2025
  4. NECTA Standard Seven Results 2025 Released: 81.8% of Candidates Pass the PSLE Examination
  5. Tarehe Mpya za Kufunguliwa Vyuo 2025/2026 Zatangazwa na Wizara ya Elimu
  6. NECTA Yatangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2025 – Asilimia 81.80 Wamefaulu Nchini
  7. Mambo 5 ya Muhimu Kujua Wakati Wa Kusubiri Kutangazwa kwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo