Jinsi ya Kukopa Salio Tigo (Menu Ya Kukopa Salio Tigo): Katika ulimwengu wa mawasiliano wa leo, kuwa na salio la kutosha kwenye simu yako ni muhimu kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki, na wafanyakazi wenzako. Lakini vipi kama salio lako litaisha ghafla na unahitaji kupiga simu muhimu au kutuma ujumbe wa dharura? Mtandao wa Tigo inatoa suluhisho la haraka kupitia huduma yake ya “kukopa salio,” ambayo inaruhusu wateja kukopa kiasi kidogo cha salio la muda wa maongezi ili kukidhi mahitaji yao ya haraka. Huduma hii ni rahisi kutumia na inaweza kuwa mkombozi katika hali zisizotarajiwa ambapo salio lako la kawaida limeisha.
Kama wewe ni mtumiaji mpya wa Tigo au ni mteja wa Tigo ambaye hujawahi kutumia huduma ya Tigo Pesa na ungependa kufahamu jinsi ya kutumia huduma hii, basi sisi Habariforum.com tutakujuza jinsi ya kukopa salio Tigo kiurahisi.
Jinsi ya Kukopa Salio Tigo (Menu Ya Kukopa Salio Tigo)
Tatizo la kukosa salio linapotokea na hauwezi kupata vocha mahali ulipo, huduma ya Tigo inakuja kukuokoa. Kukopa salio Tigo ni jambo rahisi, lakini si kila mtu anajua jinsi ya kufanya hivyo. Ikiwa wewe ni mmoja wa hao ambao hawajui jinsi ya Kukopa Salio Tigo, basi usijali. Hapa kuna mwongozo wa hatua kwa hatua kukuwezesha kukopa salio sasa.
Fuata maelekezo yaliopo chini ili uweze kupata msaada unaoutafuta bila kuteseka.
- Piga *149*05 Kisha Chagua Kifurushi unachotaka kukopa
- Huduma hii ya Niwezeshe salio itakupa salio litakalo kuwezesha kupiga simu, kutuma SMS na kuperuzi intaneti. Deni litalipwa utakapo ongeza salio.
- Piga *149*49# Kukopa Dakika Tigo
- Piga *149*55# Kukopa MB za kuperuzi intaneti
- Pia Unaweza kukopa Kifurushi chenye dakika, SMS na MB kwa kupiga *147*00#
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti