JKU vs Yanga Leo 01/05/2025 Saa Ngapi?
Timu ya wananchi Yanga SC leo tarehe 1 Mei 2025 itashuka dimbani katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU). Mchezo huu wa kusisimua umepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Gombani, uliopo kisiwani Pemba, kuanzia saa 1:15 usiku. Fainali hii inatarajiwa kuwa ya aina yake, ikileta mvutano mkali kati ya wakongwe wa Tanzania Bara na wakali wa Zanzibar.
Yanga imeingia fainali baada ya kuibuka na ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya timu ya Zimamoto katika nusu fainali ya pili ya michuano hiyo. Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja huo huo wa Gombani, na ushindani ulikuwa mkubwa kabla ya kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti. Kwa upande mwingine, JKU walijihakikishia nafasi ya kucheza fainali kwa kuifunga Azam FC kwa mabao 2-1 kwenye nusu fainali ya kwanza, ushindi ambao uliandika historia kwao.
Saa Ngapi Mechi ya JKU vs Yanga Leo Itaanza?
Mashabiki wa soka kote nchini wanatarajiwa kuifuatilia kwa karibu mechi hii ya kihistoria. Mchezo huu wa fainali kati ya Yanga SC na JKU utaanza saa 1:15 usiku katika uwanja wa Gombani, Pemba. Hii ni mechi ambayo inabeba matumaini, historia, na heshima kubwa kwa pande zote mbili.
Historia ya Kombe la Muungano
Kombe la Muungano ni mashindano yaliyobeba uzito wa kihistoria, yalianzishwa mwaka 1982 yakilenga kuimarisha mshikamano wa michezo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Michuano hii ilichezwa hadi mwaka 2002, kabla ya kusitishwa kwa muda mrefu kuanzia 2003. Hata hivyo, mwaka jana michuano hiyo ilirejeshwa rasmi, ambapo Simba SC waliibuka mabingwa baada ya kuifunga Azam FC kwa bao 1-0 katika fainali ya kihistoria.
Mwaka huu, Yanga SC inarejea kwenye fainali ikiwa na rekodi yenye mafanikio makubwa, ikisaka taji lake la saba tangu mashindano haya yaanze. Hii ni nafasi nyingine kwa Wananchi kuendeleza ubabe wao katika michuano ya Muungano. Kwa upande wa JKU, huu ni msimu wao wa kwanza kufika hatua ya fainali, na wanatafuta taji lao la kwanza katika historia ya mashindano haya.
Mapednekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Fainali Kombe La Shirikisho Afrika CAF 2024/2025
- Ratiba ya Kombe la Muungano 2025
- Kikosi cha Yanga vs Zimamoto Leo 29/04/2025
- Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025 Saa Ngapi?
- Matokeo ya Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025
- Liverpool Wafanikiwa Kuwa Mabingwa EPL 2024/2025
- Simba SC Yatinga Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Baada ya Sare na Stellenbosch
- Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025
Leave a Reply