Jonathan Sowah Kuikosa Simba vs Yanga Ngao ya Jamii Septemba 16, 2025

Jonathan Sowah Kuikosa Simba vs Yanga Ngao ya Jamii Septemba 16, 2025

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Jonathan Sowah, ataikosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC itakayopigwa tarehe 16 Septemba 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Hii ni baada ya kufungiwa kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB msimu uliopita wakati akiichezea Singida Black Stars.

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezaji anapopewa kadi nyekundu kwenye mashindano ya ndani kama FA, anatakiwa kutumikia adhabu hiyo kwenye michezo inayofuata ya ndani ikiwemo Ligi Kuu na Ngao ya Jamii. Hii inamaanisha kwamba Sowah hataruhusiwa kushiriki mchezo huo muhimu wa kufungua msimu mpya wa 2025/26.

Jonathan Sowah Kuikosa Simba vs Yanga Ngao ya Jamii Septemba 16, 2025

Pigo kwa Wekundu wa Msimbazi Simba SC

Sowah alisajiliwa katika kikosi cha wekundu wa msimbazi dirisha la usajili la kiangazi akitokea Singida Black Stars, na amehesabiwa kama moja ya silaha mpya za kocha Fadlu Davids kuelekea msimu ujao. Kukosekana kwake katika mchezo wa Ngao ya Jamii ni pigo kwa Wekundu wa Msimbazi ambao walihitaji kuonyesha ubora wa kikosi chao kipya mbele ya watani wao wa jadi Yanga.

Kwa upande wa Yanga, taarifa hii inaweza kuchukuliwa kama afueni kwani hawatakuwa na kibarua cha kumkabili mshambuliaji hatari aliyeonyesha kiwango bora msimu uliopita. Akiwa na Singida Black Stars, Sowah alifunga mabao 13 katika michezo 14, jambo lililomfanya kuwa miongoni mwa washambuliaji bora kwenye ligi.

Historia ya Jonathan Sowah

Sowah alijiunga na Singida Black Stars mwezi Januari 2025 akitokea Al Nasr ya Libya, na kabla ya hapo alikuwa akicheza katika klabu ya Medeama ya Ghana. Ni akiwa Medeama ndipo alipanza kuonekana kwenye ramani ya soka Afrika, hususan baada ya timu hiyo kukutana na Yanga katika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika msimu wa 2023/2024.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Khalid Aucho Asaini Mkataba wa Miaka 2 na Singida Black Stars
  2. Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robo fainali CHANI
  3. Timu zilizofuzu Robo Fainali CHAN 2024
  4. Simba SC Kuzindua Rasmi Jezi Mpya 2025/2026 Agosti 27
  5. Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 Zaanza Kuuzwa kwa Pre-Order – Fahamu Bei na Upatikanaji
  6. Ratiba ya Ngao ya Jamii 2025/2026
  7. Msimamo wa Ligi Kuu England EPL 2025/2026
  8. Man United Yaanza Safari ya EPL 2025/26 kwa Kupoteza Dhidi ya Arsenal
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo