Jux na Diamond Watamba na Wimbo Mpya Ololufe – Sikiliza Hapa
Goma jipya ambalo limetabiliwa kuwa jimbo la mitaa mbalimbali Tanzania na Afrika kwa ujumla limetoka rasmi, ambapo kwa mara nyingine tena Jux na Diamond Platnumz wanaungana kumuimbia mtoto mzuri Priscilla au Priscy kutoka Nigeria kama sehemu ya kuonesha jinsi gani Jux amezama katika penzi. Wimbo huu unaitwa “Ololufe” na umeanza kuvuma ndani ya saa chache tu baada ya kuachiwa, ukiwa umevuta hisia za mashabiki wa muziki wa Bongo Flavour na wengine wengi katika bara zima la Afrika.
Ushirikiano Kati ya Jux na Diamond
Kama kawaida, Jux na Diamond wameonyesha urafiki wao wa kipekee kwa kuungana na kutoa ladha tofauti katika muziki.
Hii si mara ya kwanza kwa wasanii hawa kufanya kazi pamoja, kwani walishirikiana katika goma lililovuma mno mwaka jana, “Enjoy”, ambalo lilitamba katika chati za muziki Afrika Mashariki, Magharibi, na Kati. “Enjoy” imefanikiwa kufikisha zaidi ya watazamaji milioni 90 kwenye YouTube ndani ya mwaka mmoja, na sasa “Ololufe” inaonekana kuanza na moto uleule.
Wimbo wa “Ololufe” unaonesha mchanganyiko wa sauti laini za Jux na Diamond huku wakielezea hisia zao kwa mtu wanayempenda.
Muziki huu unatumika kama zawadi kutoka kwa Jux kwenda kwa mpenzi wake mpya, Priscy, ambaye ni raia wa Nigeria. Mashabiki wa muziki wa Bongo Flavour wamesema kuwa wimbo huu umeleta mabadiliko na unawafikia watu wengi kwa muda mfupi sana.
Mapokezi Ya Wimbo wa Ololufe wa Jux Ft Diamond Platnum
Wimbo huu umeanza kwa kishindo kikubwa, ukiwa umeangaliwa zaidi ya mara laki 5 ndani ya saa 24 tangu kuwekwa kwenye mtandao wa YouTube. Mashabiki wengi wameuelezea wimbo huu kama kazi bora yenye ubunifu mkubwa, hasa kutokana na jinsi unavyoelezea mapenzi kwa hisia kali. Wakati mashabiki wa Jux wanapongeza jinsi anavyoelezea hisia zake kwa mpenzi wake mpya, wafuasi wa Diamond wanavutiwa na uwezo wake wa kufanya kazi na wasanii wengine na kuleta kitu kipya kila mara. Wimbo wa “Ololufe” unatumia lugha ya mapenzi yenye kugusa mioyo, huku sauti ya Diamond ikichangia kuongeza mvuto wa kipekee katika wimbo huo.
Jux na Diamond “Ololufe” – Sikiliza Hapa
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti