Kengold Vs Yanga Leo 25/09/2024 Saa Ngapi
Mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa kati ya KenGold na Yanga itachezwa leo tarehe 25/09/2024, kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mchezo huu ni wa aina yake kwani utawakutanisha kwa mara ya kwanza katika historia timu hizi mbili, huku Yanga ikiwa imara kutokana na ushindi mfululizo, na KenGold ikitafuta ushindi wa kwanza katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Maandalizi ya Timu ya Yanga
Yanga SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na mzuka wa hali ya juu baada ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga CBE SA ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-0 katika raundi ya pili.
Pia, mabingwa hawa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania wameanza kwa kasi msimu huu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ikishinda mechi ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 2-0. Hadi sasa, Yanga imeonekana kuwa tishio kwa wapinzani wake, huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 24 katika mechi zake saba zilizopita, ikiruhusu bao moja pekee.
Yanga pia ina rekodi nzuri ya kushinda mechi za kimataifa na za ndani, ikiwa na ubabe dhidi ya timu kama Vital’O ya Burundi na Simba SC. Kocha wa Yanga amesisitiza kuwa lengo la timu ni kuendeleza ushindi, huku wachezaji wake wakiwa kwenye kiwango cha juu kabisa.
Kwa upande mwingine, KenGold inapitia kipindi kigumu kwenye msimu wake wa kwanza Ligi Kuu. Timu hiyo imeshinda michezo yote ya awali, ikipoteza mechi nne mfululizo dhidi ya Singida Black Stars, Fountain Gate, KMC, na Kagera Sugar. Mfululizo huo wa matokeo mabaya umesababisha kocha mkuu wa timu, Fikiri Elias, kujiuzulu, na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Jumanne Challe.
Licha ya changamoto walizopitia, Challe ameweka wazi kuwa lolote linaweza kutokea katika mpira wa miguu. Alisema, “Tunajiandaa kwa mechi dhidi ya Yanga, tumejifunza mengi kutoka kwenye mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar na tutajipanga vizuri kuhakikisha tunapata matokeo chanya.”
Mchezo Utachezwa Saa Ngapi?
Mechi ya KenGold dhidi ya Yanga itaanza rasmi saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Fuatilia Hapa
Uwanja wa Mchezo
Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya, ndio utakua ulingo wa pambano hili. Ni uwanja wenye historia ya mechi kali za soka nchini Tanzania, na kwa kuwa hii ni mara ya kwanza kwa KenGold kukutana na Yanga, mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya hali ya juu.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti