Khalid Aucho Asaini Mkataba wa Miaka 2 na Singida Black Stars
Singida Black Stars imefanikiwa kukamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo tegemeo wa Yanga SC, Khalid Aucho, ambapo sasa amepewa mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo ya Singida.
Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya Aucho na Singida Black Stars yalimalizika kwa mafanikio makubwa, na tayari nyota huyo raia wa Uganda amemwaga wino. Anatarajiwa kutambulishwa rasmi muda wowote kuanzia sasa kama sehemu ya maandalizi ya kikosi kuelekea msimu wa 2025/26. Chanzo cha kuaminika kutoka klabuni Singida Black Stars kilibainisha kuwa usajili wa Khalid Aucho ni sehemu ya mikakati mikubwa ya timu hiyo, yenye lengo la kujipanga vizuri kwa mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.
“Tulipokuwa tunauza wachezaji tulikuwa na mipango mingine mikubwa ambayo siku ya Singida Big Day ndiyo tutatoa majibu kuwa bado tutakuwa na timu bora na ya ushindani. Sio Aucho tu, kuna nyota wengine bora,” kilieleza chanzo hicho.
Malengo ya Singida Black Stars
Singida Black Stars imeweka wazi kuwa kusajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa kama Aucho ni hatua ya kuimarisha kikosi na kuongeza ushindani. Viongozi wa timu hiyo wanaamini ubora wake utaleta tofauti kubwa kwenye kikosi chao, hasa kutokana na historia yake ya mafanikio ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
“Tuna malengo makubwa, kinachozingatiwa sasa ni uzoefu na ubora. Kila mmoja anafahamu ubora wa Aucho akifanya mambo makubwa kwenye ligi yetu, tunaamini atafanya hivyo pia akiwa Singida Black Stars,” kiliongeza chanzo hicho.
Kwa uzoefu alionao, Aucho anatarajiwa kuwa mchezaji kiongozi katika kikosi cha Singida Black Stars, akichangia nidhamu, uimara wa kiufundi na uongozi uwanjani.
Uzoefu wa Khalid Aucho
Khalid Aucho ana historia ndefu katika soka la Afrika na kimataifa. Alijiunga na Yanga SC mnamo Agosti 2021 akitokea Misr Lel Makkasa SC ya Misri. Katika kipindi cha misimu minne aliyocheza Jangwani, alijipatia heshima kubwa kama kiungo wa ukabaji namba moja na tegemeo la timu hiyo.
Mbali na Yanga, Aucho amecheza vilabu mbalimbali barani Afrika, Asia na Ulaya, hali inayomfanya kuwa mchezaji mwenye uzoefu wa kipekee. Timu alizowahi kuzichezea ni pamoja na:
- 2009–2010: Jinja Municipal (Uganda)
- 2010–2012: Water FC (Uganda)
- 2012–2013: Simba SC (Tanzania)
- 2013–2014: Tusker FC (Kenya)
- 2015–2016: Gor Mahia (Kenya)
- 2016: Baroka FC (Afrika Kusini)
- 2017: Red Star Belgrade (Serbia)
- 2017: OFK Beograd (Serbia)
- 2017–2018: East Bengal (India)
- 2018–2019: Churchill Brothers (India)
- 2019–2021: Misr Lel Makkasa SC (Misri)
- 2021–2025: Yanga SC (Tanzania)
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robo fainali CHANI
- Timu zilizofuzu Robo Fainali CHAN 2024
- Simba SC Kuzindua Rasmi Jezi Mpya 2025/2026 Agosti 27
- Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 Zaanza Kuuzwa kwa Pre-Order – Fahamu Bei na Upatikanaji
- Ratiba ya Ngao ya Jamii 2025/2026
- Msimamo wa Ligi Kuu England EPL 2025/2026
- Man United Yaanza Safari ya EPL 2025/26 kwa Kupoteza Dhidi ya Arsenal
- Taifa Stars Kukutana na Morocco Robo Fainali ya CHAN 2025
Leave a Reply