TFF Yatangaza Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 Morocco

Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 Morocco

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa orodha rasmi ya wachezaji walioteuliwa na kocha wa Timu ya Taifa ya wanaume, Miguel Gamondi, kuunda kikosi cha awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 zinazotarajiwa kufanyika Morocco.

Orodha hii imejumuisha wachezaji wanaocheza ndani na nje ya nchi, ikiwemo nyota wenye uzoefu mkubwa, vijana wapya wenye uwezo wa kuongeza ushindani, pamoja na wanandinga wanaoendelea kung’ara katika klabu zao za ndani na nje ya Tanzania.

Taarifa ya TFF imebainisha kuwa hatua ya awali ya kambi inalenga kufanya tathmini ya kiufundi na kuboresha uimara wa timu kabla ya kutangazwa kwa kikosi cha mwisho kitakachoshiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Gamondi ameita wachezaji wanaocheza ligi za ndani na wale wanaopata nafasi kwenye ligi za Ulaya, Asia na Amerika, jambo linaloonyesha dhamira ya kujenga timu shindani yenye mchanganyiko wa uzoefu na vipaji vipya.

Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025

  1. Hussein Masalanga – Singida Black Star
  2. Yakoub Suleiman – Simba SC
  3. Yona Amosi – Pamba Jiji FC
  4. Zuberi Foba – Azam FC
  5. Haji Mnoga – Salford City, England
  6. Iddi Selemani – Azam FC
  7. Ibrahim Abdulla – Young Africans
  8. Dickson Job – Young Africans
  9. Feisal Salum – Azam FC
  10. Cyprian Kachwele – Whitecaps FC, Canada
  11. Ahmed Pipino – KMC FC
  12. Abdul Suleiman – Azam FC
  13. Mbwana Samatta – Le Havre AC, France
  14. Morice Abraham – Simba SC
  15. Pascal Msindo – Azam FC
  16. Wilson Nangu – Simba SC
  17. Mohamed Hussein – Young Africans
  18. Lusajo Mwaikenda – Azam FC
  19. Mukrim Abdallah – Singida Black Star
  20. Nassor Saadun – Azam FC
  21. Elias Lawi – Azam FC
  22. Yusuph Kagoma – Simba SC
  23. Shomari Kapombe – Simba SC
  24. Mudahthir Yahya – Young Africans
  25. Saimon Msuva – Al-Talaba SC, Iraq
  26. Athumani Makambo – Coastal Union
  27. Vedastus Masinde – Simba SC
  28. Bakari Mwamnyeto – Young Africans
  29. Novatus Miroshi – Göztepe FC, Turkey
  30. Tarryn Allarakhia – Rochdale AFC, England
  31. Charles M’mombwa – Floriana FC, Malta
  32. Iddi Kipagwile – Dodoma Jiji
  33. Vitalis Mayanga – Mbeya City
  34. Khalid Habibu – Singida Black Star
  35. Edwin Balua – En Paralimniou, Cyprus
  36. Miano Danilo – FK Panevezys, Lithuania
  37. Alphone Mabula – FC Shamakhi, Azerbaijan
  38. Abdulkari Kiswanya – Namungo FC
  39. Abdulmalik Zakaria – Mashujaa FC
  40. Nathaniel Chilambo – Azam FC
  41. Said Khamis – Immigration FC, Malaysia
  42. Suleiman Mwalimu – Simba Sports Club
  43. Yahya Zaydi – Azam FC
  44. Offen Chikola – Young Africans
  45. Jackson Kasanzu – Tormenta FC, USA
  46. Ben Dismas – Simba SC
  47. Israel Mwenda – Young Africans
  48. Kelvin John – Aalborg BK, Denmark
  49. Kelvin Njoshi – Pamba Jiji FC
  50. Sabri Kondo – BK Häcken, Sweden
  51. Nickson Kibabage – Singida Black Star
  52. Paul Peter – JKT Tanzania
  53. Abel Josiah – JKT Tanzania U20

TFF Yatangaza Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 Morocco

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo Wa Championship Ligi Daraja la Kwanza Tanzania 2025/2026
  2. Msimamo wa Kundi la Azam Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
  3. Simba Yachezea Kichapo cha Pili Mfululizo Makundi Klabu Bingwa
  4. Singida BS Yapata Pointi ya Kwanza Makundi Kombe la Shirikisho CAF
  5. Matokeo ya Stade Malien vs Simba leo 30/11/2025
  6. Kikosi cha Simba vs Stade Malien leo 30/11/2025
  7. Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 30/11/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo