Kikosi Cha Azam Fc Vs Rayon Sports Agosti 03 2024 | Kikosi cha Azam Fc Dhidi ya Rayon Sports Mechi ya Kirafiki
Kikosi cha Azam FC kimetua salama Jijini Kigali, Rwanda, tayari kwa mpambano mkali wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao, Rayon Sports.
Mechi hii inatarajiwa kuchezwa Agosti 3, 2024, katika Uwanja wa Kigali Pelé, Nyamirambo, ikiwa ni sehemu ya tamasha kubwa la “Rayon Day.” lenye lengo kubwa la kuwaleta pamoja mashabiki wa Rayon Sports na kuwatambulisha nyota wapya waliosajiliwa.
Tamasha la Rayon Day litafanyika katika Uwanja wa Amahoro, ambao umefanyiwa marekebisho makubwa ili kuweza kuandaa mechi za kimataifa kwa kiwango cha juu. Mashabiki wa soka kutoka pande zote nchini Rwanda wanatarajiwa kuujaza uwanja huu kwa shangwe na nderemo, wakishuhudia timu hizi mbili zikichuana vikali.
Azam FC, ikiwa na kikosi chake chenye wachezaji mahiri na uzoefu, wamepania kuonyesha uwezo wao dhidi ya Rayon Sports, ambao ni mabingwa wa Rwanda. Katika m,chezo wa mwisho wa kirafiki wa Azam Fc, wanarambaramba walipokea kichapo kitakatifu kutoka kwa waydad casablanca ya Rhulani Mokwena.
Katika mechi hii dhidi ya Rayon Sports, Azam fc bilashaka atajaribu kulipa kisasi na kuwarudishia mashabiki furaha. Huu ni mtanange ambao unatarajiwa kuwa wa kusisimua, kwani timu zote mbili zina historia ya soka ya kuvutia.
Mbali na kuwa sehemu ya tamasha la “Rayon Day,” mechi hii ya Azam Fc Vs Rayon Sports pia ina umuhimu mkubwa kwa Azam FC kama sehemu ya maandalizi yao kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Baada ya kukipiga na Rayon Sports, Azam FC watakabiliana na APR FC katika mechi za hatua ya awali ya mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Kikosi Cha Azam Fc Vs Rayon Sports Agosti 03 2024
Kikosi cha Kwanza Kilichotangazwa:
- Mohamed Mustafa
- Lusajo Mwaikenda (C)
- Cheikh Sidibe
- Yeison Fuentes
- Yannick Bangala
- Adolf Mtasingwa
- Franck Tiesse
- James Akaminko
- Jhonier Blanco
- Fei Toto
- Gibril Sillah
Wachezaji wa Akiba: Foba, Sebo, Chilambo, Msindo, Yoro, Samake, Meza, Nado, Saadun, Tepsie, Diakite, Adam
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day
- Cv Ya Moussa Camara Kipa Mpya Wa Simba 2024/2025
- Kamati Mpya Ya Mashindano Simba Sc 2024/2025 Yatangazwa
- Wasanii Watakao Tumbuiza Simba Day 2024
- Washindi wa Tuzo za TFF 2023/2024
- Hizi Apa Picha za Jezi Mpya ya Azam Fc 2024/2025
- Opah Clement Ajiunga Na Henan Fc Ya Ligi Kuu Ya China
Weka Komenti