Kikosi cha Coastal Union Vs Bravos do Maquis Leo 17/08/2024 Kombe la Shirikisho CAF | KIkosi cha Coastal Union Leo
Wagosi wa Kaya, Coastal Union, leo tarehe 17 Agosti 2024, wanatarajia kuanza rasmi kampeni yao ya kimataifa kwa kupambana na Bravos do Maquis ya Angola katika mchuano wa kufuzu hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF 2024/2025. Mchezo huu utafanyika katika uwanja wa Estadion Nacional, uliopo Lubango, Angola, ukianza rasmi majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Coastal Union, inarejea tena kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miongo mitatu. Mara ya mwisho timu hii kushiriki katika michuano hii ilikuwa mwaka 1989, hivyo ushindi katika mchezo huu wa leo unamaanisha mengi kwao, si tu kwa kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofuata, bali pia kwa kuendeleza hadhi yao katika medani ya soka la kimataifa.
Coastal Union ilifanya maandalizi kabambe kuelekea mchezo huu muhimu, ikizingatia ukubwa wa jukumu walilokabiliana nalo. Kocha mkuu wa timu hiyo, pamoja na benchi lake la ufundi, walijikita zaidi katika kuboresha mbinu za kiufundi na kiufundi ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya katika uwanja wa ugenini. Timu ilielezwa kuwa na ari na mori wa hali ya juu, ikilenga kumaliza mchezo huu mapema na kuweka msingi mzuri kwa mchezo wa marudiano utakaofanyika Tanga.
Kikosi cha Coastal Union Vs Bravos do Maquis Leo 17/08/2024 CAF
Wakati tunasubiri kikosi rasmi cha Coastal union leo ambacho kinatarajiwa kutangazwa saa moja kable ya mchezo kuanza, habariforum tumejaribu kutabiri kikosi cha wagosi wa kaya kitakacho anza katika mchezo huu wa kombe la shirikisho Afrika.
- Chuma
- Jackson
- Miraji
- Issa
- Abdallah
- Semfuko
- Denis
- Ramadhani
- John
- Lucas
- Hernest
Substitutes: Athumani, Cosmas, Salum, Mbaraka, Greyson, Bakari, Gift, Kulumba, Jeremie
Fuatilia Hapa Matokeo Ya Bravos do Maquis Vs Coastal Union Leo 17/08/2024
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti