Kikosi cha Simba SC vs TRA United Leo 09/04/2026
Wekundu wa Msimbazi leo watakuwa ugenini kuzisaka pointi tatu muhimu katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, ambapo Simba SC itashuka dimbani dhidi ya TRA United kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Mchezo huu wa kiporo uliosogezwa mbele kutokana na mvua kubwa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku timu zote zikiwa na malengo tofauti ya matokeo.
Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa imetoka kuangusha pointi mbili mbele ya Azam, jambo linaloongeza presha ya kutafuta ushindi ili kurejea kwenye mwenendo mzuri. Kwa upande wa TRA United, timu hiyo inaingia uwanjani ikiwa na dhamira ya kuvunja rekodi mbaya dhidi ya Simba, ambayo haijawahi kuizuia tangu ipande Ligi Kuu.
Rekodi zinaonyesha kuwa kabla ya mchezo huu, timu hizo zimekutana mara tano na Simba ikishinda zote huku ikifunga mabao 15. TRA United haijawahi kufunga bao hata moja katika mikutano hiyo, hali inayoweka presha kwa wenyeji kuelekea mchezo huu wa sita.
Hata hivyo, Simba imekuwa na changamoto kwenye michezo ya ugenini msimu huu. Katika mechi tano zilizopita ugenini, imeshinda mbili dhidi ya Tanzania Prisons (2-0) na Singida Black Stars (2-1), huku ikitoa sare tatu dhidi ya Dodoma Jiji (1-1), Pamba Jiji (1-1) na Azam (0-0).
Habari njema kwa Simba ni kurejea kwa winga Elie Mpanzu, aliyekosa michezo miwili iliyopita kutokana na kuumwa. Mpanzu ana nafasi ya asilimia 50 ya kucheza katika mchezo huu, akiwa kinara wa kutengeneza mabao kwa asisti tano sawa na Feisal Salum wa Azam FC msimu huu.
Kocha wa Simba, Steve Barker, amesema wanatarajia mchezo mgumu dhidi ya TRA United lakini wamejipanga kurejea kwenye ushindi.
“Utakuwa mchezo mgumu, tunakutana na TRA United inayocheza mpira mzuri, ina wachezaji wenye nguvu na kutokana na mchezo wa kwanza kuahirishwa na tulipowafunga nyumbani itaufanya mchezo huu kuwa na presha yake lakini tunataka kushinda turudi kwenye njia ya ushindi,” alisema Barker.
Kwa upande wa TRA United, timu hiyo chini ya kocha Ettiene Ndayiragije imekuwa na matokeo mazuri ya nyumbani ikiwa imeshinda mechi tatu kati ya tano, sare moja na kupoteza moja. Hata hivyo, itawakosa Chamou Karaboue na Mzamiru Yassin kutokana na masharti ya mikataba yao ya mkopo kutoka Simba.
Ndayiragije amesema wataingia uwanjani kwa mkakati wa kuzuia ubora wa Simba na kutumia makosa yao ili kupata ushindi. “Simba ni moja kati ya timu kubwa hapa Tanzania, ina wachezaji wenye uzoefu mkubwa lazima uwe na hesabu nzuri, tutajaribu kuzuia yale ambayo yanawapa ubora lakini pia tutumie makosa yao kuweza kutengeeneza ushindi wetu,” alisema Ndayiragije.
Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya TRA United
Mashabiki wa wekundu wa Msimbazi wanasubiria kwa hamu kuona orodha ya wachezaji ambao benchi la ufundi la Simba litawaamini katika mchezo huu wa leo. Kwa kawaida, katika michezo ya Ligi Kuu, vikosi vya kwanza hutangazwa rasmi saa moja kabla ya mchezo kuanza.
Hiki Apa Kikosi cha Simba kilichotangazwa
Kabla ya mchezo huo, Bodi ya Ligi Tanzania ilitoa taarifa kuhusu mashabiki waliokata tiketi za mchezo uliokuwa umeahirishwa Machi 14, ikieleza kuwa wataingia kwa tiketi hizo hizo bila kununua mpya, mradi wawe na kadi walizotumia awali. Wale ambao hawakununua tiketi katika mchezo wa kwanza wanatakiwa kununua tiketi mpya kwa mechi ya leo.
Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi, presha ya matokeo na hali ya timu zote kuelekea kwenye hatua hii ya msimu
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
- Matokeo ya Pamba Jiji vs Yanga Leo 08/04/2026
- Harry Maguire Asaini Mkataba Mpya Manchester United Hadi 2027
- AFCON 2027 Kufanyika Mwezi Juni na Julai
- Droo ya Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza: Man City Yapangwa na Southampton, Chelsea Uso kwa Uso Dhidi ya Leeds
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali FA Cup Pemba









Leave a Reply