Kikosi Cha Simba Vs Al Ahly Tripoli Leo 15 September 2024 | Kikosi cha Simba Leo Vs Al Ahly Tripoli | Kikosi cha Simba Dhidi ya Al Ahly
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo watakua nchini Libya kupambana na Al Ahly Tripoli katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2024/2025. Hii ni mechi muhimu kwa Simba ambayo ina historia nzuri katika mashindano ya kimataifa, huku Al Ahly Tripoli ikiwa ni timu yenye mafanikio makubwa kwenye soka la Libya.
Al Ahly Tripoli ni moja ya klabu zenye mafanikio zaidi nchini Libya, ikiwa imeshinda mataji 13 ya Ligi Kuu ya Libya na mataji 7 ya Kombe la Libya. Pia ni klabu pekee kutoka Libya iliyowahi kufika fainali ya michuano ya Afrika mwaka 1984.
Katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mafanikio yao makubwa ni kufika nusu fainali mwaka 2022. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1950 ikijulikana kama Al Istiqlal, lakini baadaye ikabadilishwa kuwa Al Ahly Tripoli.
Kabla ya kukutana na Simba, Al Ahly Tripoli imefuzu hatua hii baada ya kuitoa timu ya Uhamiaji ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 5-1. Katika michezo hiyo miwili, Al Ahly ilishinda mechi zote, ikifunga mabao 2-0 na 3-1. Ushindi huu unathibitisha uwezo wao wa kucheza katika mashindano ya kimataifa, huku timu yao ikijivunia nyota kama Ahmed Krawa’a na Ammar Taifour walioonyesha uwezo mkubwa.
Kikosi Cha Simba Vs Al Ahly Tripoli Leo 15 September 2024
Katika mchezo huu muhimu wa Simba dhidi ya Al Ahly, matarajio ni makubwa kwa mashabiki wa Simba. Wengi wanatamani kuona kikosi bora zaidi cha Simba kikipambana uwanjani ili kuhakikisha ushindi wa mapema. Kocha Faldu Davis anatarajiwa kutangaza rasmi kikosi kitakachoanza majira ya saa moja usiku, na tutakuwa hapa kukuletea orodha kamili.
Kikosi Cha Simba SC:
- 40 Camara
- 12 Kapombe
- 15 Hussein
- 14 Hamza
- 20 Che Malone
- 21 Kagoma
- 37 Balua
- 17 Fernandes
- 13 Ateba
- 10 Ahoua
- 26 Mutale
Wachezaji wa Akiba (Subs): Ally, Kujili, Chamou, Ngoma, Okejapha, Kibu, Awesu, Mkwala & Mashaka
Kocha Wa Simba Akizungumzia Kikosi cha Simba Vs Al Ahly Tripoli Leo na Mechi Kiujumla
Kocha Fadlu akizungumzia maandalizi ya kikosi kuelekea mchezo wa kesho. #WenyeNchi #NguvuMoja pic.twitter.com/CcrHwtW7m2
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) September 14, 2024
Mabadiliko Makubwa Simba SC 2024/2025
Simba inashuka uwanjani ikiwa na kikosi kipya na kikubwa kilichofanyiwa maboresho makubwa kuelekea msimu wa 2024/2025.
Chini ya uongozi wa mwekezaji Mohamed Dewji, Simba imejizatiti kuhakikisha inafika mbali zaidi katika mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania msimu uliopita.
Simba ilifanya usajili wa wachezaji nyota kutoka ndani na nje ya nchi. Baadhi ya majina mapya katika kikosi cha Simba ni pamoja na Jean Charles Ahoua, mshindi wa tuzo ya MVP ya Ligi Kuu ya Ivory Coast, Karaboue Chamou kutoka Ivory Coast, na mshambuliaji Stephen Mukwala kutoka Uganda. Wachezaji hawa wapya wana matumaini makubwa ya kuimarisha kikosi cha Simba kinachoongozwa na kocha Fadlu Davids.
Katika michezo ya mwanzo ya Ligi Kuu ya Tanzania msimu huu, Simba imeanza kwa kishindo, ikishinda mechi zake mbili za kwanza kwa mabao 7-0 dhidi ya Tabora United na Fountain Gate.
Jean Charles Ahoua ameanza msimu kwa kiwango bora, akihusika moja kwa moja katika mabao manne kati ya saba yaliyofungwa na Simba, jambo linalowapa mashabiki matumaini makubwa ya ushindi katika mechi ya leo dhidi ya Al Ahly Tripoli.
Changamoto Zinazomkabili Simba
Al Ahly Tripoli imejizatiti kwa kufanya usajili wa wachezaji wengi wenye uzoefu, wakiwemo nyota tisa wapya, lakini tano kati yao wana umri wa zaidi ya miaka 30. Miongoni mwa wachezaji hao ni mshambuliaji Mabululu, anayelipwa mshahara wa dola 50,000 kwa mwezi. Mabululu alifunga mabao 11 msimu uliopita akiwa na Ittihad Alexandria ya Misri, na atakuwa tishio kubwa kwa safu ya ulinzi ya Simba.
Licha ya ubora wa wachezaji wa Al Ahly Tripoli, Simba inaweza kutumia udhaifu wa timu hiyo kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa kwa kuwasukuma kasi na kuwakimbiza uwanjani. Pia, Simba ina faida ya kuwa na kikosi kipana na vijana wenye ari kubwa ya kupambania matokeo bora, licha ya changamoto ya uzoefu wa wachezaji wa Al Ahly.
Matarajio ya Mchezo
Mchezo huu utakaochezwa katika Uwanja wa June 11, Tripoli, unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa. Simba ina nafasi nzuri ya kupata matokeo mazuri, hasa kutokana na rekodi yake ya kufika hatua za juu za michuano ya CAF katika miaka ya hivi karibuni.
Ushindi leo utaiweka Simba katika nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano utakaofanyika Jumapili, 22 Septemba 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mashabiki wa Simba wana matarajio makubwa na wachezaji wapya kama Jean Charles Ahoua, Stephen Mukwala, na Mousa Camara, ambao tayari wameonyesha kiwango bora katika michezo ya awali ya Ligi Kuu ya Tanzania.
Kwa upande mwingine, Al Ahly Tripoli inajivunia uzoefu na mafanikio katika mashindano ya kimataifa, lakini changamoto yao kubwa ni kucheza dhidi ya timu yenye kasi kama Simba, ambayo inakuja na ari mpya ya kushinda.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba Vs Al Ahly Tripoli Leo – Saa Ngapi Mechi Inaanza?
- Ratiba ya Mechi za Leo 15 September 2024
- Haaland Avunja Rekodi ya Rooney ya Magoli EPL
- Azam Fc Yaambulia Sare ya 0-0 Mbele ya Pamba Jiji
- Man U Yaishushia Southampton Kichapo cha Goli 3-0
- Tabora United Yashindwa Kutamba Nyumbani
- Yanga Yaanza na Ushindi Ethiopia, Dube Aingia Wavuni
Weka Komenti