Kikosi cha Simba VS Es Tunis Leo 1/02/2026
Leo saa 10:00 jioni, klabu ya Simba SC itashuka dimbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikaribisha Esperance de Tunis (ES Tunis) kwenye mechi ya marudiano ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huu ni wa kuamua hatima ya Simba katika mashindano hayo msimu wa 2025/2026, kwani matokeo yoyote tofauti na ushindi yatamaanisha safari yao inafikia tamati mapema.
Mechi hiyo itarushwa mbashara kupitia AzamSports1HD, na inatarajiwa kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa Simba ambao wamejipanga kuijaza Benjamin Mkapa kwa lengo la kuisapoti timu yao katika pambano hili gumu.
Umuhimu wa Mechi kwa Simba
Kwa Simba, mchezo huu si wa kawaida. Ni mtihani wa mwisho wa kuendelea kubaki na matumaini ya kusonga mbele. Simba tayari ilipoteza mechi ya kwanza ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Esperance, matokeo ambayo sasa yameiweka katika hali ya lazima kushinda.
Ushindi wa leo utakuwa na maana mbili kubwa:
- Kulipiza kisasi cha kipigo cha mchezo wa kwanza.
- Kufufua matumaini ya kufuzu robo fainali, ingawa bado itahitajika kushinda mechi mbili zilizosalia na pia kuombea matokeo ya timu nyingine yawe na faida kwao.
Iwapo Simba itashindwa kupata pointi tatu leo, basi itakuwa imeaga rasmi Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Mwamuzi na Wasaidizi Wake
Shirikisho la soka barani Afrika limempa jukumu la kusimamia mchezo huu refa Celso Alvacao kutoka Msumbiji. Atasaidiwa na:
- Zacarias Baloi – Msaidizi wa kwanza
- Venestancio Cossa – Msaidizi wa pili
- Simoes Guambe – Mwamuzi wa nne
Uwepo wa waamuzi hawa wa kimataifa unalenga kuhakikisha haki inatendeka ndani ya uwanja.
Fuatilia Hapa Kikosi cha Simba VS Es Tunis Leo 1/02/2026
Kikosi cha Simba kitakachoanza leo dhidi ya ES Tunis kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9 alasiri, saa moja kabla ya kuanza kwa mchezo huo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Tangazo hilo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Simba, kutokana na uzito wa mechi na mabadiliko yaliyofanyika ndani ya kikosi katika dirisha dogo la usajili.
Kwa kuzingatia mazingira ya mchezo na hitajio la lazima la kupata ushindi, benchi la ufundi linatarajiwa kuwa litachagua kikosi chenye wachezaji wenye uzoefu na nguvu mpya watakaoweza kuipa timu ponti tatu muhimu. Simba ina wigo mpana wa wachezaji baada ya kuwasajili nyota sita wa kigeni ambao wameongeza ushindani katika nafasi mbalimbali uwanjani.
Nguvu Mpya Ndani ya Kikosi cha Simba
Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa na maboresho makubwa ya kikosi baada ya kusajili nyota sita wa kigeni katika dirisha dogo la usajili. Wachezaji hao ni:
- Jospin Loemba
- Libasse Gueye
- Anicet Oura
- Clatous Chama
- Djibrilla Kassali
- Ismael Toure
Usajili huu unatarajiwa kuongeza ushindani na ubora ndani ya kikosi, hasa katika eneo la ushambuliaji na kiungo, ambako Simba inahitaji kuwa makini zaidi katika kutumia nafasi.
Kauli ya Kocha Steve Barker
Kocha wa Simba, Steve Barker, amesema wazi kuwa mechi ya leo ni ya lazima kushinda, vinginevyo wataaga mashindano.
“Tunajua kwamba tunacheza dhidi ya timu nzuri. Tunaamini kwamba bado nafasi yetu ipo ya kusonga mbele ukizingatia tutakuwa nyumbani na tutakuwa na sapoti ya mashabiki wetu.”
Barker aliongeza kuwa siri ya ushindi ni kutumia vizuri nafasi:
“Ili tupate ushindi tunatakiwa kuimarika hasa katika kutumia nafasi. Tunatakiwa kutengeneza sana nafasi na tunafahamu kwamba katika Ligi ya Mabingwa Afrika huwa hakuna timu rahisi.”
Kauli hizi zinaonesha wazi kuwa Simba inalijua uzito wa mchezo na imejiandaa kisaikolojia kwa mapambano makali.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply