Kikosi cha Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Kagera Sugar Ligi Kuu
Mnyama Simba SC leo tarehe 22 Juni 2025 atakua mawindoni kuzisaka pointi tatu muhimu atakapo wakabili walima sukari wa Kagera Sugar katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2024/2025.
Huu ni mchezo wa raundi ya 30, ukiwa na maana kubwa kwa Simba SC, ambaye hadi sasa anashikilia nafasi ya pili akiwa na pointi 75, pointi moja nyuma ya kinara Yanga SC. Kwa Simba, ushindi ni lazima ili kuendeleza matumaini ya ubingwa kuelekea mchezo wao wa mwisho dhidi ya Yanga, mchezo unaotarajiwa kuwa fainali ya kuamua bingwa wa msimu huu.
Katika kuhakikisha ushindi leo, Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amewataka wachezaji wake kutimiza majukumu maalumu kwa nidhamu ya hali ya juu. Kocha huyo ambaye ametua Msimbazi msimu huu akitokea Raja Casablanca ya Morocco, amebadilisha kabisa sura ya timu, akiifanya kuwa mpinzani mkubwa wa Yanga tofauti na matarajio ya awali ya baadhi ya wadau wa soka.
Katika maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa leo, Fadlu amewapa nafasi ya dakika 90 mastaa wake wa kikosi cha kwanza, akiwemo kinara wa mabao Jean Charles Ahoua, kiungo mahiri Ellie Mpanzu, na mshambuliaji tegemeo Steven Mukwala. Lengo ni kumalizana na Kagera Sugar kabla ya kuhamishia nguvu kwa mchezo wa mwisho wa msimu dhidi ya mahasimu wao wa jadi Yanga SC.
Kikosi cha Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025
Kikosi rasmi cha Simba kitakachoshuka dimbani leo dhidi ya Kagera Sugar kinatarajiwa kutangazwa rasmi saa 09:00 alasiri.
Hadi sasa, wachezaji wa kikosi cha kwanza kama Jean Charles Ahoua, Steven Mukwala, na Ellie Mpanzu wanatarajiwa kuanza mechi hii muhimu kutokana na umuhimu wake kwenye muktadha wa ubingwa. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee, ukizingatia nafasi kubwa iliyo mbele ya Simba SC katika historia ya ligi msimu huu.
Simba SC: Lengo ni Pointi Tatu Muhimu
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, Simba SC inahitaji ushindi dhidi ya Kagera Sugar ili kubaki kwenye mbio za ubingwa. Kocha Fadlu amesisitiza kuwa licha ya ushindi wa mabao 5-0 walioupata dhidi ya KenGold katika mechi iliyopita, kikosi chake kinapaswa kuongeza ufanisi wa matumizi ya nafasi, hususan katika mechi mbili zilizobaki.
Aliweka bayana kuwa mashambulizi ya timu bado yanahitaji uboreshaji. Katika mchezo uliopita, Ahoua alipoteza nafasi tatu wazi licha ya kufunga bao moja, jambo lililompa Kocha sababu ya kudai ukomavu zaidi mbele ya lango. Hali hiyo, kwa mujibu wa Fadlu, haiwezi kuvumiliwa leo dhidi ya Kagera wala kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga.
Kagera Sugar: Bila Presha, Lakini si wa Kubezwa
Pamoja na kuwa tayari imeshuka daraja, Kagera Sugar haipaswi kubezwa. Fadlu Davids ameonya kuwa timu kama hizi hucheza kwa uhuru zaidi kwa sababu hazina shinikizo la kusaka alama. Hili linaifanya kuwa hatari zaidi kwa Simba, ambao wako chini ya presha kubwa ya matokeo. Kwa mantiki hiyo, Simba italazimika kucheza kwa umakini mkubwa katika safu zote ulinzi, kiungo na ushambuliaji.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?
- Yanga vs Dodoma Jiji Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?
- TFF Yafunga Rasmi Zoezi la Uchukuaji wa Fomu za Uongozi – Wagombea 25 Wajitokeza
- Tanzania Yashinda Ubingwa wa CECAFA Wanawake 2025 Kupitia Twiga Stars
- KMKM Mabingwa wa FA Cup Zanzibar 2025 Baada ya Ushindi wa 4-2 Dhidi ya Chipukizi
- Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Klabu ya Liverpool Yamwaga Mamilioni Kumnasa Florian Wirtz
- Viingilio Simba SC vs Kagera Sugar 22/06/2025
Leave a Reply