Kikosi cha Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025

Kikosi cha Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025

Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakua dimbani kuzisaka pointi tatu muhimu za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026 mbele ya wageni wao Namungo FC katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam majira ya saa 2:15 usiku.

Huu ni mchezo unaotajwa kuwa na uzito mkubwa kwa timu zote mbili ambazo zinahitaji kuimarisha nafasi zao katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi msimu huu.

Kikosi cha Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025

Simba SC: Kuelekea Mchezo wa Leo

Simba SC inashuka uwanjani ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya Namungo, ambapo katika mechi 12 za Ligi Kuu walizokutana, Wekundu wa Msimbazi wameshinda michezo saba na kutoka sare mara tano bila kupoteza hata mmoja. Pia, katika michezo miwili ya mwisho msimu uliopita, Simba iliibuka na ushindi nyumbani na ugenini kwa mabao 3-0 bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa.

Akizungumza kuelekea mchezo huu, Kocha Msaidizi Seleman Matola, ambaye kwa sasa anaongoza kikosi cha Simba kufuatia kuondoka kwa Fadlu Davids, amesema hawatarajii mchezo mwepesi.

“Tunatarajia kuwa na mechi ngumu, kama mkiangalia rekodi, Namungo wamekuwa wakitusumbua licha ya kuwafunga mechi mbili za mwisho. Wana kocha mzuri anayeifahamu Simba, tutaingia na tahadhari kubwa,” alisema Matola.

Matola ameongeza kuwa changamoto kubwa kwa Simba imekuwa ni kukosa umakini katika kumalizia nafasi walizokuwa wakizipata, jambo ambalo amesema tayari limefanyiwa kazi.

“Tunalijua hilo kwani tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi shida imekuwa kuzimalizia, tumelifanyia kazi kwa kiwango kikubwa,” alisisitiza.

Simba imeanza kampeni zake za ligi msimu huu kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate, jambo linaloongeza morali ya wachezaji wake kuelekea pambano la leo.

Namungo FC: Changamoto ya Mkapa

Kwa upande wa Namungo FC, kikosi hicho kinashuka dimbani kikiwa na morali ya kutopoteza katika michezo miwili ya awali ya ligi msimu huu. Walifungua kampeni kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Pamba Jiji na kisha wakapata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema maandalizi ya kikosi chake kwa siku tatu zilizopita jijini Dar es Salaam yamekuwa ya kiwango cha juu, na lengo ni kupambana kwa nguvu dhidi ya Simba licha ya kutambua ugumu wa mchezo.

“Tuna siku tatu hapa mjini, tumejiandaa vizuri kuja kukutana na timu nzuri, yenye wachezaji wazuri, maandalizi yote tumeyafanya ili tufanye vizuri. Tuhaiheshimu Simba, tumekuja kushindana nao,” alisema Mgunda.

Hata hivyo, historia haipo upande wa Namungo kwani katika michezo yote 13 ya mashindano waliyokutana na Simba, hawajawahi kupata ushindi. Simba imeshinda mara nane na kutoka sare mara tano, huku kumbukumbu mbaya zaidi kwa Mgunda ikiwa msimu uliopita aliposhuhudia timu yake ikipoteza kwa mabao 3-0 mara mbili dhidi ya Simba.

Mbali na Ligi Kuu, timu hizi zilikutana pia Januari 1, 2021 katika mchezo wa Kombe la FA ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Rekodi hizi zinaonyesha wazi ugumu wa Namungo kupata matokeo mazuri dhidi ya Wekundu wa Msimbazi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025 Saa Ngapi?
  2. Singida BS Yaendeleza Ubabe Mbele ya Mashujaa na Kubaki Kinara wa Ligi Kuu Bara
  3. Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  4. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  5. Viingilio Mechi ya Simba vs Namungo FC 01/10/2025
  6. Yanga Sc Yalazimishwa Sare Ya 0-0 Na Mbeya City
  7. Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
  8. Arsenal yapata ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Newcastle United
  9. Wapinzani wa Simba Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika CAF
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo