Kikosi cha Simba Vs Yanga Ngao Ya Jamii | Kikosi cha Simba Dhidi ya Yanga
Baada ya Kumalizika kwa michezo ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya, Hatimaye Simba sc inarejea katika michezo ya msimu wa 2024/2025 rasmi uku wakianza msimu kwa kuwakabili waasimu wao wa muda mrefu na mabingwa wa ligi kuu ya NBC kwa mara tatu mfululizo Yanga Sc katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya jamii. Mechi hii inayotarajiwa kua ya aina yake imepangwa kuchezeka majira ya saa 01 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam na inatarajiwa kua mechi ngumu na yenye mvuto mkubwa.
Simba Sc Yalenga Kulipa Kisasi
Kuelekea mchezo huu, Simba Sc inalenga kulipa kisasi kufuatia vipigo viwili vya mbwa koko walivyopata kutoka kwa Yanga Sc katika msimu uliopita. Katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC, Simba walishishiwa kipigo cha mwizi cha 5-1, na katika mechi ya raundi ya pili, Yanga walishinda 2-1. Ushindi wa Yanga katika mechi zote mbili umewacha Simba na kiu ya ushindi katika mchezo huu wa Ngao ya Jamii.
Kauli za Makocha na Wachezaji
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, ameweka wazi kuwa wanauchukulia mchezo huu kwa uzito mkubwa. “Tunaichukulia mechi hii kama mechi nyingine tunayohitaji kushinda ili kuanza vizuri msimu kwa kulitetea kombe hili,” alisema Davids. “Nina uzoefu wa michezo hii mikubwa ya dabi, ukiangalia timu yetu ni mpya tutakuja na mbinu tofauti kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.”
Nahodha wa Simba, Mohamed Hussein, pia ameonyesha matumaini kuelekea mchezo huo. “Kulingana na maandalizi tuliyoyafanya timu yetu imeimarika zaidi ila tunaamini tunaenda kukutana na timu yenye wachezaji wazuri, utakuwa mchezo wenye ushindani ila malengo yetu ni kupata ushindi,” alisema Hussein.
Kikosi cha Simba Vs Yanga 08/08 2024 Ngao Ya Jamii
Angalia Hapa Kikosi cha Yanga Vs Simba Ngao Ya Jamii 08/08/2024
Fuatilia Haoa Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024
Uchambuzi wa Mchezo
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na historia ya upinzani kati ya timu hizi mbili. Yanga Sc, wakiwa mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC mara tatu mfululizo, watakuwa wakijitahidi kudumisha ubora wao, huku Simba Sc wakitafuta kulipa kisasi na kuanza msimu mpya kwa ushindi.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania wana kila sababu ya kutarajia burudani ya hali ya juu katika mtanange huu wa Ngao ya Jamii. Je, Simba Sc watafanikiwa kulipa kisasi, au Yanga Sc wataendeleza ubabe wao? Jibu litapatikana uwanjani tarehe 8 Agosti.
Soma Hapa Kikosi cha Yanga Vs Simba Ngao Ya Jamii 08/08/2024
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti