Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa kambini Kuelekea COSAFA na Mechi ya Kirafiki
Wakati michuano ya COSAFA inakaribia kuanza kutimua vumbi, timu ya Taifa ya mprira wa miguu Tanzania almaharufu kama taifa stars teari imesha anza mipango ya kuingia kambini ili kujieka sawa na nmichuano hio pamoja na mechi ya kirafiki dhidi ya Bafana Bafana (Afrika Kusini). Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini kuanzia tarehe 2 Juni 2025. Kikosi hiki kimeteuliwa maalum kwa ajili ya maandalizi ya mechi hizo mbili muhimu zitakazotoa taswira ya uwezo wa timu ya taifa kuelekea mashindano yajayo.
Katika mashindano ya COSAFA, Tanzania imepangwa kucheza dhidi ya Eswatini na Madagascar. Hii ni nafasi adhimu kwa kocha Hemed Suleiman kufanya tathmini ya kina kuhusu viwango vya wachezaji wake, hasa wale wanaochipukia pamoja na wale wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Majina ya Wachezaji Walioitwa Kikosini Taifa Stars Kujiandaa na COSAFA & Bafana Bafana
Kocha Hemed Suleiman amewaita jumla ya wachezaji 30 kutoka klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Kikosi hiki kimejumuisha wachezaji chipukizi pamoja na mastaa wanaofanya vizuri kwenye ligi mbalimbali. Hawa hapa ni wachezaji walioteuliwa:
Walinda Mlango:
- Yakoub Suleiman – JKT Tanzania
- Ally Salim – Simba SC
- Hussein Masaranga – Singida BS
Mabeki:
- Antony Remmy – Azam FC U20
- Mirajy Abdallah – Coastal Union
- Shomari Kapombe – Simba SC
- Lusajo Mwaikenda – Azam FC
- Vedastus Masinde – TMA Stars FC
- Wilson Nangu – JKT Tanzania
- Mohamed Hussein – Simba SC
- Ibrahim Ame – Mashujaa FC
Viungo:
- Pascal Msindo – Azam FC
- Alphonse Mabula – Shamakhki FC (Azerbaijan)
- Ibrahim Abdulla – Young Africans
- Dickson Job – Young Africans
- Abdulahrahim Bausi – JKT Tanzania
- Idrisa Sitambuli – Mashujaa FC
- Abdulrazack Mohamed – Simba SC
- Ahmed Pipino – KMC FC
- Yusuph Kagoma – Simba SC
- Sheikhan Khamis – Young Africans
- Feisal Salum – Azam FC
Washambuliaji:
- Valentino Mshaka – Simba SC
- Kibu Denis – Simba SC
- Ismail Msuyu – Al-Talaba SC (Iraq)
- Iddy Selemani – Azam FC
- Mishano Daudi – Kengold FC
- Selemani Mwalimu – Wydad Casablanca (Morocco)
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025
- Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025 Saa Ngapi?
- Coastal Union Yapiga Hesabu Kali Kumchukua Anicet Kiazayidi
- Chelsea Yaipiga Bao Manchester United Usajili wa Liam Rory Delap
- Xabi Alonso Aahidi Kurejesha Ufalme wa Real Madrid
- Singida BS Yashindwa Kutamba Mbele ya Simba Ligi Kuu NBC
- Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa!
- Erik Ten Hag Atambulisha Rasmi Kama Kocha Mkuu Bayer Leverkusen
Leave a Reply