Kikosi cha Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025

Kikosi cha Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo kinarejea dimbani katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya AFCON 2025, kikibeba matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora. Stars itachuana vikali na Tunisia katika mchezo wenye presha kubwa, ambapo matokeo yake yataamua hatma ya safari ya Tanzania katika michuano hiyo. Mechi hii ya Kundi C itapigwa kuanzia saa 1:00 usiku katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah Olympique Annexe mjini Rabat na kurushwa mubashara kupitia AzamSports1HD.

Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda ‘The Cranes’, Taifa Stars imejikuta katika hesabu ngumu za kufuzu. Matokeo hayo yaliifanya Tanzania kubaki na pointi moja pekee, hali inayolazimisha ushindi wa lazima dhidi ya Tunisia, sambamba na kuitegemea Nigeria ‘Super Eagles’ iifunge Uganda katika mechi nyingine ya kundi hilo.

Kikosi cha Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025

Hesabu za kufuzu Kundi C

Kundi C tayari linaongoza Nigeria, ambayo imeshafuzu hatua ya 16 bora baada ya kushinda mechi zake zote mbili. Super Eagles ilianza kwa kuifunga Taifa Stars mabao 2-1, kabla ya kuiondoa Tunisia kwa ushindi wa mabao 3-2.

Kwa upande wa Tunisia, kikosi hicho kimepata matokeo magumu baada ya kufungwa mechi moja na kutoka sare mechi nyingine, hali inayoifanya pia ihitaji ushindi ili kuendelea kubaki kwenye mchakato wa kufuzu.

Kwa Taifa Stars, ushindi dhidi ya Tunisia leo ni sharti lisilojadiliwa. Sare au kufungwa kutamaanisha safari ya Tanzania kuishia hatua ya makundi, huku ushindi ukifungua dirisha la matumaini, hasa iwapo Nigeria itaendeleza ubabe wake dhidi ya Uganda.

Kikosi cha Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025

Kikosi rasmi cha timu ya Tanzania Taifa Stars kitakachoanza leo dhidi ya Tunisia kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 12 jioni.

Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanasubiri kwa hamu kuona nyota watakaopewa dhamana ya kuipigania Taifa katika mechi hii nyeti ya AFCON 2025. Kwa kuzingatia presha ya ushindi wa lazima, matarajio ni kwamba kocha Miguel Gamondi atachagua kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu na nguvu, kikiongozwa na wachezaji walio onesha ubora wao katika mechi zilizopita za Kundi C.

Kumbukumbu ya mechi ya Tanzania dhidi ya Uganda

Katika mchezo wa juzi dhidi ya Uganda, Stars ilionyesha nia ya kupambana baada ya Simon Msuva kuipatia Tanzania bao la kuongoza dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti. Bao hilo liliamsha matumaini ya ushindi, lakini Uganda ilisawazisha dakika ya 80 kupitia Uche Ikpeazu. Uganda pia ilikosa penalti ya dakika ya 90, iliyopigwa na Allan Okello, na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kocha Miguel Gamondi alifanya mabadiliko muhimu katika mchezo huo kwa kumtoa Kelvin John na Tarryn Allarakhia, nafasi zao zikichukuliwa na Dickson Job pamoja na Mbwana Samatta. Mabadiliko hayo yaliifanya Stars kubadilisha mfumo wa uchezaji na kutumia mabeki watatu, wakiongozwa na Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na Dickson Job.

Mfumo huo uliwapa nafasi Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Haji Mnoga kusaidia ulinzi na mashambulizi, lakini Uganda iliendelea kuwa hatari kupitia mashambulizi ya pembeni na mipira mirefu, ambayo hatimaye ilizaa bao la kusawazisha.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
  2. Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Uganda Leo 27/12/2025
  3. Matokeo ya Uganda Vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025
  4. Uganda vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025 Saa Ngapi?
  5. Ratiba ya Mechi za AFCON Leo 27/12/2025
  6. Msimamo wa Makundi AFCON 2025
  7. Bao la Dakika za Mwisho la Patson Daka Lainusuru Zambia Dhidi ya Mali, Mechi Ikiisha 1-1
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo