Kikosi cha Yanga SC vs Tanzania Prisons Leo 04/04/2026
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, kinatarajiwa kushuka dimbani leo kukabiliana na Tanzania Prisons katika mchezo muhimu wa ligi utakaopigwa majira ya saa 12:30 jioni katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona Kikosi cha Yanga SC vs Tanzania Prisons Leo 04/04/2026, huku timu zote mbili zikiingia uwanjani zikiwa na presha ya matokeo kutokana na mwenendo wao wa hivi karibuni.
Kikosi kinachotarajiwa cha Yanga SC leo
Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa na baadhi ya changamoto kikosini, ikiwemo kukosekana kwa kipa wake namba moja Djigui Diarra ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu.
Hata hivyo, kikosi hicho kinabaki na nyota wake muhimu wakiongozwa na mshambuliaji Laurindo Dilson Maria ‘Depu’, aliyefunga bao la ushindi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons.
Katika benchi la ufundi, kocha Pedro Goncalves ataendelea kutegemea wachezaji wake wa msingi licha ya matokeo ya sare tatu mfululizo zilizopita.
Kocha msaidizi wa timu hiyo, Matthew Silva, alisema maandalizi ya timu yako vizuri licha ya matokeo hayo:
“Tunatambua kiu ya mashabiki wetu ni kuona tunashinda… tutapambana ili kupata matokeo mazuri.”
Kikosi cha Tanzania Prisons leo
Kwa upande wa Tanzania Prisons, kikosi kinachoongozwa na kocha Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ kinatarajiwa kuingia uwanjani kikiwa na lengo la kusaka ushindi muhimu ili kujinasua kutoka nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi.
Prisons imekuwa katika kipindi kigumu baada ya kushindwa kushinda mechi nne mfululizo, hali inayowalazimu wachezaji kuonyesha nidhamu na kujituma zaidi katika mchezo wa leo.
Kocha Nsajigwa alieleza wazi mkakati wa timu yake kuelekea mchezo huo:
“Tutacheza kwa nidhamu kubwa ya kujilinda, lakini wakati huohuo tukiwashambulia pia kwa kuwashtukiza.”
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Sc Kilichotangazwa leo
Rekodi za timu zote kabla ya mchezo
Yanga SC:
- Haijapoteza mechi 36 za Ligi Kuu
- Imeshinda mechi 30 na sare 6 katika rekodi hiyo
- Msimu huu: mechi 16, ushindi 11, sare 5 (pointi 38)
Tanzania Prisons:
- Nafasi ya 15 kwenye msimamo
- Pointi 13 baada ya mechi 17
- Ushindi 3, sare 4, kupoteza 10
Takwimu hizi zinaonyesha wazi tofauti ya ubora wa timu hizi, lakini presha ya matokeo inaweza kufanya mchezo huu kuwa wa ushindani mkubwa.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply