Kikosi cha Yanga vs JS Kabylie Leo 28/11/2025
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC leo watakuwa ugenini kutunishiana misuli na JS Kabylie ya Algeria katika mchezo muhimu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku kukiwa na matarajio makubwa kwa mashabiki na presha ya ushindani ikiongezeka kadri dakika zinavyosonga. Hii ni safari nyingine yenye uzito mkubwa kwa wawakilishi hao wa Tanzania ambao wanarejea Algeria kwa lengo moja kutafuta pointi tatu muhimu katika mbio za kuwania nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.
Kikosi cha Yanga, kilicho katika Kundi B, kinaingia kwenye pambano hili kikiwa na motisha ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat katika mchezo wa ufunguzi. Kocha Pedro Gonçalves amesisitiza kuwa, licha ya kukutana na wapinzani wenye rekodi nzuri wakiwa nyumbani, kikosi chake “kimejipanga kushtua wenyeji kwa nidhamu ya juu na mashambulizi ya kushtukiza.”
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na benchi la ufundi, Yanga imefanya safari ya mapema kuelekea Algeria kwa lengo la kuzoea hali ya hewa ya baridi kali pamoja na mvua ya barafu iliyoanza kunyesha katika siku za maandalizi.
Pedro alieleza kuwa mazoezi mfululizo katika mazingira hayo yametoa nafasi kwa wachezaji “kuzoea mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa” na kuweka mwili tayari kwa changamoto ya leo usiku.
Historia na Rekodi Kati ya Timu
Safari ya Yanga kuelekea Algeria imekuwa na ladha mchanganyiko katika misimu ya hivi karibuni. Baada ya ushindi wa kihistoria dhidi ya USM Alger Juni 2023, Yanga ilipata matokeo magumu katika michezo miwili iliyofuata nchini humo—ikifungwa 3-0 na CR Belouizdad (2023) na baadaye kushindwa 2-0 dhidi ya MC Alger (2023).
Kwa upande mwingine, JS Kabylie inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na rekodi nzuri sana nyumbani. Katika michezo 17 ya CAF tangu Januari 5, 2021, imeshinda 13, sare 3 na kupoteza mchezo mmoja pekee. Msimu huu imeanza kwa kupiga mabao 5-0 dhidi ya Bibiani Gold Stars na 2-1 dhidi ya US Monastir, ikionesha ubora wake inapocheza mbele ya mashabiki wake.
Mbinu, Muundo wa Kikosi na Maandalizi ya Yanga
Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji, alithibitisha kuwa wachezaji 22 walisafiri huku wote wakiwa katika hali nzuri kiafya. Hakuna hata mmoja katika waliobaki Dar es Salaam aliyehusika katika mchezo wao uliopita, jambo linaloashiria kuwa kocha Pedro ana kikosi chake kamili. Pedro amekuwa akisisitiza umuhimu wa eneo la kiungo, ambalo ameliita injini ya timu kutokana na wachezaji kama Duke Abuya, Mudathir Yahya, Mohamed Doumbia, Mousa Balla Conte, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli. Uwepo wa wachezaji hawa wenye uzoefu mkubwa unatarajiwa kuwa nguzo muhimu dhidi ya mchezo wa nguvu na kasi wa JS Kabylie.
Katika mahojiano ya awali, Pedro alibainisha kuwa leo anategemea mbinu za counter-attack zenye nguvu “mara tu tutakapofanikiwa kupokonya mpira,” akiamini kwamba kasi ya wachezaji wa mbele na nidhamu ya ulinzi inaweza kuleta matokeo mazuri.
Kikosi cha Yanga vs JS Kabylie Leo 28/11/2025
Mashabiki wengi wa Yanga SC wanatazamia kwa hamu kuona orodha ya wachezaji ambao Kocha Pedro Gonçalves atawapangia majukumu katika mchezo wa leo dhidi ya JS Kabylie. Kama ilivyo desturi katika michezo ya kimataifa ya CAF, kikosi cha kwanza hutangazwa rasmi saa moja kabla ya mchezo kuanza.
Hivyo basi, kikosi rasmi cha Yanga SC dhidi ya JS Kabylie Leo 28/11/2025 kitapangwa na kuthibitishwa na benchi la ufundi saa moja kabla ya kipenga cha kwanza kupulizwa. Tutakuleta taarifa kamili ya Kikosi cha Yanga vs JS Kabylie Leo 28/11/2025 mara tu kitakapotangazwa rasmi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- TFF Yatangaza Kuahirishwa kwa Tuzo za Msimu 2024/2025
- Timu Tatu za Tanzania Zashindwa Kung’ara Katika Michezo ya Kwanza ya Makundi CAF
- Msimamo wa Makundi Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
- Msimamo Kundi la Simba Klabu Bingwa 2025/2026
- Matokeo ya Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025
- Wachezaji Wanaowania Tuzo za TFF 2024/2025









Leave a Reply