Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 – Toyota Cup

Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 – Toyota Cup | Kikosi cha Yanga Dhidi ya Kaizer Chiefs

Yanga SC itakutana na Kaizer Chiefs tarehe 28 Julai 2024 katika mchezo wa Toyota Cup. Mchezo huu utafanyika katika Uwanja wa Toyota Stadium, Bloemfontein saa 9 alasiri kwa saa za Afrika Kusini na saa 10 jioni kwa saa za Tanzania. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia baina ya timu hizi mbili ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa katika soka.

Kikosi cha Timu ya wananchi Yanga kimeonesha kiwango cha juu katika mechi mbili za Mpumalanga Premier International Cup. Katika mechi hizo, Yanga ilishinda mechi moja dhidi ya TS Galaxy kwa ushindi mwembamba wa goli 1-0 na kupoteza moja dhidi ya FC Ausburg ya Ujerumani kwa matokeo ya 2-1. Hata hivyo, Yanga haikuwa na nyota wake muhimu, Pacome Zouzou, katika michezo hiyo.

Kaizer Chiefs nao wamefanya mabadiliko makubwa katika kikosi chao, ikiwa ni pamoja na kumsajili Nasreddine Nabi kama kocha mpya na kuongeza wachezaji wenye viwango vya juu. Mabadiliko haya yameongeza hamasa na matarajio kwa mashabiki wa timu hiyo.

Pambano hili kali kati ya mabingwa wa soka Tanzania, Yanga SC, na wababe wa Afrika Kusini, Kaizer Chiefs, linatarajiwa kuwa la aina yake, huku hamasi ikizidi kupanda na kua juu zaidi baada ya Kaizer Chiefs kutangaza kuuza tiketi zote 46,000 za mchezo huu.

Uwanja wa Toyota Stadium, Bloemfontein, unatarajiwa kujaa pomoni, mashabiki wakiwa tayari kushuhudia burudani ya hali ya juu kutoka kwa timu hizi mbili zenye historia ndefu ya ushindani. Hapa tutakuletea kikosi rasmi cha Yanga Sc dhidi ya Kaizer Chiefs mara baada ya kutangwa. Pia wakati tukisubili kocha wa Yanga atangaze safu ya kikosi cha Yanga tumekuletea orodha ya wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuwepo katika kikosi cha Yanga Sc Vs Kaizer Chiefs

Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 – Toyota Cup

Huku kocha mkuu wa Yanga, Miguel Ángel Gamondi, akitarajiwa kutangaza kikosi rasmi cha Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs nusu saa kabla ya mechi hii kuanza, tumekuletea kikosi kinachowezekana kuanza kulingana na utabiri wa wachambuzi wa soka.

Kikosi Rasmi Cha Yanga Dhidi ya Kaizer

  1. 39 DIARRA
  2. 21 YAO
  3. 30 KIBABAGE
  4. 5 D.JOB (C)
  5. 4 BACCA
  6. 9 AUCHO
  7. 38 DUKE
  8. 7 MAXI
  9. 24 CLEMENT
  10. 10 AZIZ KI
  11. 29 DUBE

Wachezaji Wa Ziada: Khomeny, Mshery, Mwamnyeto, Aziz A, Kibwana, Nkane, Farid, Sureboy, Jonas, Shekhan, Mudathir, Chama, Pacome, Musonda, Baleke

Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 - Toyota Cup

Kikosi Cha Kaizer Chief Dhidi ya Yanga Sc

1 Petersen
39 Frosler
24 Ditlhokwe
25 Msimango
34 Mbuthu
8 Maart (©)
37 Zwane
42 Shabalala
28 Vilakazi
9 Du Preez
7 Chivaviro

Wachezaji wa Ziada: Bvuma, Ntwari, Mthethwa, Castillo, Saile, Radebe, Ngcobo, Kwinika, Duba, Ozoemena, Jansen, Mmodi & Dortley

Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 - Toyota Cup

Taarifa Zaidi Kuhusu Mechi ya Yanga Vs Kaizer Chiefs

🏆#ToyotaCup
⚽️Kaizer Chiefs vs. Young Africans SC
👕First Team
🗓️Sunday 28 July 2024
🏟Toyota Stadium, Bloemfontein
🕞15h00
🎟R60 & R40 – Ticketpro, Spar – http://linktr.ee/kaizerchiefs

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Yapata Mserereko CAF: Mechi Zote za Klabu Bingwa Kupigwa Dar es Salaam
  2. Matokeo TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki
  3. Kikosi cha Yanga Vs TS Galaxy 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki
  4. Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo