Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025

Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Pamba Jiji Ligi Kuu ya NBC 2025/2026

Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025

Timu ya Wananchi Yanga leo itaanza rasmi kampeni yake ya kulitetea taji la Ligi Kuu NBC Tanzania msimu wa 2025/26, katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo watakuwa wenyeji wa Pamba Jiji FC. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Jumatano, Septemba 24, 2025, kuanzia saa 1:00 usiku na utarushwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD.

Wananchi wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na morali ya juu baada ya kuanza mechi zao za kwanza kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 ugenini nchini Angola dhidi ya Wiliete SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ule ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba. Ushindi huo si tu uliwahakikishia tiketi ya kusonga mbele kimataifa, bali pia uliwapatia zawadi ya shilingi milioni 15 kutoka CAF.

Kwa upande wa ligi ya ndani, Yanga inaanza safari ya zaidi ya miezi minane ya kutafuta kutwaa ubingwa kwa mara ya tano mfululizo. Rekodi zinaonyesha kuwa timu hiyo haijapoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu katika mechi 20 mfululizo, ikishinda michezo 19 na kutoka sare moja pekee. Kocha Romain Folz atakuwa kwenye benchi kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye Ligi Kuu, akitarajiwa kupanga kikosi imara kitakachohakikisha wanaanza kampeni kwa ushindi.

Wapinzani wa leo, Pamba Jiji FC kutoka Mwanza, wanaingia uwanjani baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wao wa kwanza wa msimu. Bao pekee kwa Pamba Jiji lilifungwa na Staphan Siwa dakika ya 19, kabla ya kuruhusu Namungo kusawazisha dakika ya 90+7.

Kocha Francis Baraza, anayejulikana kwa falsafa ya soka la kushambulia, amesisitiza kuwa hana hofu ya kuwakabili mabingwa watetezi. Baraza amesema wachezaji wake watapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao endapo wataepuka makosa ya kimsingi, akiongeza kuwa timu yake iko tayari kuleta ushindani mkubwa.

Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025

Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025

Kuelekea mchezo huu wa kwanza wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/26, mashabiki wa soka nchini wanasubiri kwa hamu orodha ya wachezaji watakaopangwa kuanza na benchi la ufundi la Yanga SC dhidi ya Pamba Jiji FC. Kama ilivyo ada ya michezo mikubwa, kikosi cha kwanza hutangazwa rasmi saa moja kabla ya mpira kuanza.

Hapa Habariforum tutakuletea mara moja kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 kitakapowekwa wazi na benchi la ufundi cha Wananchi, pamoja na taarifa zote muhimu zitakazohusiana na mchezo huu.

Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025

Waamuzi wa Mchezo

Mchezo wa leo utaongozwa na refa Abdul Wajihi, akisaidiwa na Janeth Balama na Omari Juma, huku refa wa akiba akiwa Isihaka Mwalile. Waamuzi hawa wanatarajiwa kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki na nidhamu ya hali ya juu.

Hitimisho: Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 kinatarajiwa kuamua mwanzo wa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu NBC Tanzania. Kwa upande mmoja, Wananchi wanaanza kwa shauku ya kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza na kulinda taji, huku kwa upande mwingine Pamba Jiji wakisaka matokeo ya kuvunja rekodi na kujijengea heshima. Dakika 90 za mchezo huu zinaahidi burudani kubwa kwa mashabiki wa soka nchini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 Saa Ngapi?
  2. Ratiba ya Mechi za Leo 24/09/2025
  3. Fadlu Davids Atambulishwa Kama Kocha Mkuu wa Raja Casablanca ya Morocco
  4. Lamine Yamal Abeba Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka (Kopa Trophy)
  5. Simba Yamtambulisha Hemed Suleiman Kama Kocha wa Mpito
  6. Ousmane Dembélé Ashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025
  7. Viwango Vya FIFA Duniani 2025 (FIFA Rankings)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo