Kikosi cha Yanga Vs Red Arrows Leo Agosti 03 2024 | Kikosi cha Yanga Dhidi ya Red Arrows Leo Mechi ya Kirafiki
Baada ya Tamasha la #SimbaDay2024 kukamilika hapo jana Agosti 03 kwa Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya APR FC ya Rwanda, leo Agosti 4 mashabiki na wadau wa soka watashuhudia tukio lingine la kihistoria la Yanga Day 2024. Tamasha la Simba lilifanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambapo maelfu wa mashabiki waliujaza uwanja huo wakipata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na kushuhudia kikosii kipya cha Simba kikiisulubu APR katika mechi ya kirafiki. Katika mchezo huo dhidi ya APR magoli ya Simba yaliwekwa wavuni na Debora Fernandez (46) na Edwin Balua (66)
Simba ikiwa na kikosi cha wachezaji wengi ambao ni wapya kikosini hapo imewapa furaha mashabiki wake ambao asilimia kubwa waliujaza Uwanja huo kuanzia Saa 10 Jioni ya leo Agosti 3, 2024. Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kuelekea kuanza kwa msimu ujao wa 2024/25
Leo ni zamu ya mashabiki wa wapinzani wa Simba, Yanga Sc kuonesha ubora wao wa kulijaza dimba la benjamin mkapa ambapo klabu yao inatambulisha kikosi kipya, jezi mpya na msimu mpya kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Kombe la Kagame 2024, Red Arrows ya Zambia kujiweka sawa kwa msimu mpya kwa klabu hiyo iliyotimiza miaka 89 tangu iliposisiwa mwaka 1935.
Kikosi cha Yanga Vs Red Arrows Leo Agosti 03 2024 – Yanga Day
Klabu ya Yanga leo inatarajiwa kushuka dimbani kuikabili Red Arrows katika mchezo wa kirafiki utakao chezeka katika dimba la Benjamin Mkapa. mchezo huu unasubiriwa kwa hamu zaidi haswa na mashabiki wa Yanga ambao wamekua na mwanzo mzuri wa maandalizi ya msimu wa 2024/2025 baada ya kikosi cha timu yao kuonesha ubora mkubwa katika michezo ya kirafiki iliochezeka Afrika kusini.
Katika mchezo huu wa yanga dhidi ya Red Arrows, tunategemea kocha wa Yanga Miguel Gamand kuanzisha kikosi bora ili kupata ushindi mnene ambao utahitimisha siku hii ya kihistoria kwa Yanga kwqa furaha iso na kifani. Hapa Habariforum tutakuletea kikosi rasmi icha Yanga vs Red Arrows mara tu baada ya kutangazwa na kocha mkuu wa Yanga.
Wakati tukisubiri kikosi rasmi cha Gamond kutangawa, hapa chini tumekuletea kikosi ambacho wachambuzi wengi wanatarajia kitaanza katika mchezo huu wa leo. Kikosi hiki kimepangwa kutokana na ubora ambao wachezaji hawa wameonesha katika michezo iliopita.
Utabiri wa Kikosi cha Yanga Dhidi ya Red Arrows Leo
- 39 Diarra
- 21 Yao
- 30 Kibabage
- 5 D.Job (C)
- 4 Bacca
- 9 Aucho
- 38 Duke
- 7 Maxi
- 24 Clement
- 10 Aziz Ki
- 29 Dube
Fuatilia Matokeo ya Yanga Vs Red Arrows Leo Agosti 03 2024 Hapa
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa wa kusisimua sana. Yanga, wakiwa na kikosi kipya kilichoimarishwa na wachezaji wenye uzoefu kutoka Simba na Azam, watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Red Arrows, mabingwa wa Kombe la Kagame.
Mashabiki wa Yanga wana matumaini makubwa na kikosi chao kipya. Wachezaji wapya kama Cloutus Chama na Prince Dube wanatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji ya Yanga. Hata hivyo, Red Arrows nao si wababe wa kubezwa. Wakiwa mabingwa wa Kombe la Kagame, wameonyesha uwezo mkubwa katika michuano ya kimataifa.
Mechi hii dhidi ya Red Arrows ni kipimo muhimu kwa Yanga kujiandaa kwa msimu mpya. Red Arrows, ambao ni mabingwa wa Kombe la Kagame 2024, ni timu yenye uwezo mkubwa na itatoa changamoto nzuri kwa Yanga kujipima nguvu.
Yanga Day ni siku muhimu kwa klabu ya Yanga na mashabiki wake. Ni fursa ya kusherehekea mafanikio ya klabu na kuangalia mbele kwa matumaini katika msimu mpya ambao unatarajiwa kuanza rasmi Agosti 08 kwa mechi dhidi ya Simba Sc.
Kwa historia na rekodi zake, Yanga inabaki kuwa klabu ya pekee na yenye hadhi kubwa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mashabiki wanatarajia kuona maonyesho bora kutoka kwa kikosi kipya na burudani safi katika mchezo wa leo dhidi ya Red Arrows.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi
- Matokeo ya Simba Vs APR Leo 03 Agosti 2024 – Simba Day
- Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day
- Simba Day 2024 LIVE: Ubaya Ubwela, Mkapa Yafurika Mashabiki
- Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo 28/07/2024 – Toyota Cup
- Matokeo TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki
- Matokeo ya Yanga vs FC Augsburg Leo 20 Julai 2024: Yaliyojiri Uwanjani
Weka Komenti