Kikosi cha Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB | Kikosi cha Yanga leo Dhidi ya Singida BS
Timu ya Wananchi, Yanga SC, leo tarehe 29 Juni 2025, itashuka tena dimbani kuwania kutwaa taji la CRDB Federation Cup katika fainali itakayochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, saa 2:15 usiku.
Hii inakuja siku chache tu baada ya kutetea kwa mafanikio ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC kwa kuifunga Simba SC mabao 2-0 tarehe 25 Juni 2025, na hivyo kuhitimisha kampeni yao ya ligi kwa mafanikio makubwa.
Katika fainali ya leo, Yanga SC itamenyana na Singida Black Stars kwenye mchezo wa kihistoria unaotazamwa kama zaidi ya pambano la kawaida, hasa kwa makocha wa timu hizo – Miloud Hamdi wa Yanga na David Ouma wa Singida Black Stars.
Kikosi cha Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB
Kikosi rasmi cha Yanga SC dhidi ya Singida Black Stars kinatarajiwa kutangazwa rasmi saa moja usiku, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo. Hata hivyo, mashabiki wanatarajia kuona baadhi ya wachezaji wao tegemeo ndani ya kikosi hicho, wakiwemo:
- Clatous Chama
- Pacome Zouzoua
- Clement Mzize
Wachezaji kama Pacome Zouzoua na Clement Mzize wamekuwa chachu ya mafanikio ya Yanga SC katika msimu huu, kila mmoja akiwa na mabao zaidi ya 10 katika orodha ya wafungaji bora wa ligi. Wameonesha ubora wao katika mechi muhimu, na leo wanatarajiwa tena kuonesha makali yao katika fainali hii.
Kwa upande wa Singida Black Stars, bado haijabainika rasmi ni wachezaji gani watapangwa, lakini bila shaka kocha Ouma atatoka na kikosi imara kinacholenga kuleta ushindani mkubwa dhidi ya mabingwa wa ligi.
Kocha Miloud Hamdi: Dhamira ya Kuandika Historia Mpya
Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi, ambaye alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo mwezi Februari 2025, anatazama fainali hii kama fursa ya kuweka historia binafsi na ya klabu. Akizungumza kabla ya mazoezi ya mwisho yaliyopangwa kufanyika saa 12 jioni, Hamdi alieleza kuwa ushindi wa leo utamuwezesha kutwaa mataji mawili makubwa ndani ya msimu mmoja hatua ambayo Yanga iliwahi kuifikia chini ya kocha wa zamani, Miguel Gamondi.
“Fainali hii kwangu inamaanisha tunakwenda kushinda makombe mawili, tayari tumeshinda ligi na sasa tukishinda hii maana yake ni makombe mawili,” alisema Hamdi.
“Kombe ni sehemu ya mafanikio ya klabu, Yanga ni klabu ya kushinda makombe, hivyo kwangu sio tu kucheza fainali, nipo hapa kwa ajili ya kushinda.”
Hamdi ana matumaini makubwa kwa kikosi chake, ambacho kimejijengea jina kwa kushinda mataji mara kwa mara katika misimu iliyopita.
David Ouma na Singida Black Stars: Safari ya Kipekee ya Kihistoria
Kwa upande wa kocha wa Singida Black Stars, David Ouma, fainali hii ni hatua ya mafanikio binafsi na ya timu. Ouma, ambaye ni raia wa Kenya, aliiongoza Coastal Union hadi hatua ya nusu fainali msimu uliopita kabla ya kutolewa na Azam FC kwa mabao 3-0.
Safari hii akiwa na Singida Black Stars, amefanikiwa kuvuka hadi fainali – mafanikio makubwa kwa klabu hiyo ambayo ilibadilishwa jina mapema mwaka 2024 kutoka Ihefu FC kuwa Singida Black Stars.
“Nikiwa Coastal Union, msimu uliopita tuliishia nusu fainali katika Kombe la FA, lakini sasa hapa Singida Black Stars tumeingia fainali,” alisema Ouma.
“Nataka kuona tunashinda kikombe na kuweka historia mpya ndani ya klabu hii.”
Kwa kuzingatia uwekezaji mkubwa uliofanyika ndani ya klabu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa kisasa huko Mtipa, Ouma anaamini kuwa ushindi katika fainali hii utakuwa zawadi bora kwa mashabiki na wadau wa timu hiyo.
Rekodi na Historia ya FA: Yanga Bado Ndio Mbabe wa Michuano Hii
Kwa mujibu wa takwimu za michuano ya Kombe la Shirikisho (CRDB Federation Cup), Yanga SC ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa zaidi tangu michuano hiyo irejee rasmi msimu wa 2015/2016.
Hadi sasa, Yanga tayari imelitwaa taji hili mara nne, ikifuatiwa na Simba SC mara tatu, Mtibwa Sugar mara moja, na Azam FC pia mara moja. Kwa upande wa Singida Black Stars, hii ni fursa yao ya kwanza kucheza fainali ya aina hii, hivyo ushindi utakuwa wa kihistoria.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB Saa Ngapi?
- Chelsea Yajipanga Kuzima Moto wa Di Maria Katika Mechi ya Usiku Dhidi ya Benfica
- Simba Yavizia Saini ya Issa Fofana Nchini Ivory Coast Kama Mrithi wa Camara
- Ratiba ya CHAN 2024/2025 | CAF African Nations Championship
- Ratiba ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Hatua ya 16 Bora
- Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Wydad Casablanca Yafungashiwa Virago Kombe la Dunia Bila Pointi
- Asante Kotoko Yachukua Nafasi ya Yanga Kombe la Toyota Afrika Kusini
Leave a Reply