Klabu ya Singida Black Star Yamtambulisha Rasmi Victorien Adebayor
Klabu ya soka ya Singida Black Star imetangaza rasmi usajili wa mshambuliaji mahiri, Victorien Adebayor. Usajili huu unakuja baada ya tetesi za muda mrefu zilizomhusisha mchezaji huyo na klabu ya Simba, ambazo hazikuzaa matunda.
Adebayor, ambaye pia ana rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Niger, anajiunga na Singida Black Star akiwa mchezaji huru baada ya kuitumikia klabu ya AS GNN ya Niger. Mshambuliaji huyu mwenye uzoefu amewahi pia kucheza katika klabu mbalimbali duniani, ikiwemo Amazulu ya Afrika Kusini, HB Köge ya Denmark, Ennpi ya Misri, na RS Berkane ya Morocco.
Hussein Masanza, msemaji wa Singida Black Star, amethibitisha kuwasili kwa Adebayor nchini Tanzania. Masanza alieleza kuwa mchezaji huyo alichelewa kidogo kuripoti kambini kutokana na dharura zisizoepukika, hali ambayo imeathiri kidogo maandalizi yake ya msimu mpya. Hata hivyo, Masanza alionyesha imani kubwa katika uwezo wa Adebayor kufikia kiwango cha wachezaji wenzake na kuwa msaada mkubwa kwa timu.
“Adebayor ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ambaye amekuwa akifanya vizuri katika ligi ya Nigeria,” alisema Masanza. “Tunatambua kwamba usajili wake ulikuwa na ushindani mkubwa, lakini shukrani kwa timu yetu ya uchunguzi (scout) iliyofanikisha kumpata.”
Masanza aliongeza kuwa Singida Black Star ina matumaini makubwa kwamba Adebayor atakuwa mchezaji bora na mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2024/25.
Usajili wa Adebayor unatajwa kuwa ni hatua kubwa kwa Singida Black Star katika kujenga kikosi imara kitakachoweza kushindana vikali katika Ligi Kuu na michuano mingine. Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanasubiri kwa hamu kumuona mshambuliaji huyo akitamba uwanjani akiwa na jezi ya Singida Black Star.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Usajili wa Mukwala na Ahou Waanza Kulipa Msimbazi
- Usajili wa Chelsea 2024/2025
- Dirisha la usajili Tanzania 2024/2025 Kufungwa Leo Agosti 15
- Mashujaa FC Yafunga Dirisha la Usajili kwa Kumnasa Kibaya
- TETESI ZA USAJILI: Dodoma Jiji FC Katika Mazungumzo ya Kumrejesha Wazir Jr
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
Weka Komenti