KMC Vs Simba Leo 11/02/2026 Saa Ngapi?

KMC Vs Simba Leo 11/02/2026 Saa Ngapi?

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wanatarajiwa kushuka dimbani leo wakikabiliana na KMC katika mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), mchezo unaosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka nchini. Timu hizo zitachuana jijini Dar es Salaam huku mashabiki wakitafuta kujua ratiba kamili ya pambano hilo pamoja na maandalizi ya kikosi cha Simba kuelekea mchezo huo muhimu.

KMC Vs Simba Leo Saa Ngapi?

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi, mchezo kati ya KMC na Simba SC utapigwa Jumatano, Februari 11, 2026 saa 1:00 usiku kwa muda wa Tanzania katika uwanja wa KMC Complex, ambao ni uwanja wa nyumbani wa KMC.

Mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja kupitia AzamSports1HD.

Siku hiyo hiyo pia kuna mchezo mwingine wa ligi ambapo Singida BS watacheza dhidi ya Fountain Gate saa 10:00 jioni katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jambo linalokamilisha ratiba ya mechi za siku hiyo ya NBC Premier League.

Soma Pia:

  1. Mechi ya Yanga vs Kabylie CAF ni Lini? Tarehe, Saa na Mahali
  2. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  3. Kocha wa Yanga Pedro Gonçalves Ashinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Januari

KMC Vs Simba Leo 11/02/2026 Saa Ngapi?

Maandalizi ya Simba SC kuelekea Mchezo

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameelezea hali ya maandalizi ya kikosi chake kabla ya mtanange huo, akisisitiza umuhimu wa kuingia uwanjani kwa kiwango cha juu.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, kocha huyo amesema maandalizi yamekwenda vyema na timu iko tayari kwa ushindani.

“Tunahitaji kucheza mechi hii vizuri ikiwa ni pamoja na kutawala mchezo na kupata ushindi kama ambavyo malengo yetu yalivyo,” amesema Barker.

Kauli hiyo inaashiria dhamira ya kikosi hicho kuendelea kuonyesha ushindani mkubwa, hasa katika kipindi ambacho kinatafuta kuimarisha mwenendo wake wa matokeo ndani ya ligi.

Simba Inaingia na Malengo ya Kuendeleza Matokeo

Simba SC inaingia katika pambano hilo ikiwa na hamasa ya kuendeleza mfululizo wa matokeo mazuri pamoja na kuimarisha nafasi yake katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchezo dhidi ya KMC unatazamwa kuwa sehemu ya safari ya kufikia malengo hayo, huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkali ndani ya dakika 90 za mchezo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Al Nasr Yafikia Makubaliano Rasmi na Simba SC Kumnunua Kibu Denis
  2. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 CAF
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo