Kocha Mpya Wa Simba Steve Barker Atambulishwa Leo Desemba 19, 2025
Klabu ya Simba SC, leo Ijumaa Desemba 19, 2025, imemtangaza rasmi Steve Barker kutoka Afrika Kusini kuwa Kocha Mpya Wa Simba. Barker mwenye umri wa miaka 57 anajiunga na Simba akitokea klabu ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, aliyokuwa akiinoa kabla ya uteuzi huo.
Steve Barker anawasili Simba akiwa na rekodi ya hivi karibuni ya mafanikio katika mashindano ya Afrika, baada ya kuiongoza Stellenbosch kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu uliopita. Katika hatua hiyo, Stellenbosch ilikutana na Simba SC.
Katika msimu huu, Kocha Mpya Wa Simba Steve Barker, ambaye alizaliwa nchini Lesotho, ameiongoza Stellenbosch katika jumla ya mechi 24 za mashindano mbalimbali. Katika mechi hizo, timu ilipata ushindi mara nane, sare sita na kupoteza mechi kumi.
Kabla ya kuinoa Stellenbosch, Barker amewahi kuzifundisha klabu za Mpumalanga Black Aces, AmaZulu pamoja na Chuo Kikuu cha Pretoria. Amejulikana kama kocha anayeheshimika kwa mchango wake katika kukuza vipaji vya vijana na ujenzi wa timu zenye nidhamu pamoja na mtindo wa kisasa wa kucheza.
Steve Barker anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dimitar Pantev, ambaye Simba SC iliachana naye Desemba 2, 2025 kwa makubaliano ya pande mbili. Uamuzi huo ulifuatia matokeo yasiyoridhisha katika mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Katika mechi hizo, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Petro Atletico na kufungwa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Stade Malien. Baada ya matokeo hayo, Simba ipo mkiani mwa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi ya kwanza ya Kocha Mpya Wa Simba Steve Barker kuiongoza Simba katika mashindano ya kimataifa itakuwa dhidi ya Esperance de Tunis ya Tunisia.
Kwa upande wake, Barker anaondoka Stellenbosch akiiacha timu hiyo ikiwa nafasi ya 14 kati ya timu 16 katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini, hali inayoiweka karibu na eneo la kushuka daraja. Barker alijiunga na Stellenbosch mwanzoni mwa msimu wa 2017–2018, na aliiongoza klabu hiyo kutwaa taji lao la kwanza la ndani kupitia Kombe la Carling Knockout msimu wa 2023–2024. Mkataba wake na Stellenbosch ulikuwa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Uteuzi wa Barker unamfanya kuwa kocha wa tatu kuinoa Simba SC msimu huu, baada ya Fadlu Davids na Dimitar Pantev.
Mapendekzo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mechi za Taifa Stars AFCON 2025
- Taifa Stars Tayari kwa AFCON 2025 Baada ya Kuwasili Morocco
- CV Ya Steve Barker Kocha Mpya wa Simba 2025/2026
- Bei ya Tiketi za Kombe la Dunia 2026 Yazua Mjadala Mkubwa Duniani
- Mchango Mkubwa wa Salah Waipa Liverpool Ushindi Mnono Dhidi ya Brighton
- Timu Nane Zathibitishwa Kushiriki Kombe la Mapinduzi 2026 Zanzibar
- Ratiba Ya AFCON 2025 Hatua Ya Makundi








Leave a Reply