Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 Kuanza September 17 2025
Baada ya mashabiki wa soka kusubiri kwa muda mrefu tangazo rasmi la siku ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026, hatimaye leo Agosti 29, 2025 Bodi ya Ligi kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imethibitisha kwamba ligi hiyo itaanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 17, 2025. Tangazo hili limeleta msisimko mkubwa kwa mashabiki wa soka kote nchini, huku wengi wakijiandaa kushuhudia burudani na ushindani wa kiwango cha juu katika viwanja mbalimbali.
Mchezo wa Ufunguzi: KMC FC vs Dodoma Jiji
Katika ratiba iliyowekwa, mchezo wa kwanza wa msimu utafanyika jijini Dar es Salaam ambapo KMC FC watakabiliana na Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa KMC Complex. Wakati huo huo, Coastal Union kutoka Tanga watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Mchezo huu nao unatarajiwa kuvutia mashabiki wa soka, hasa kutokana na nafasi ya Coastal Union kuanza msimu wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki wao.
Simba SC na Yanga SC kuanza baadaye
Kwa mujibu wa TFF, mechi za vigogo wa soka nchini Young Africans SC na Simba SC hazitachezwa katika wiki ya kwanza ya ligi kutokana na majukumu ya kimataifa ya CAF.
- Yanga SC watacheza dhidi ya Mtibwa Sugar baadaye mwezi Oktoba 2025.
- Simba SC wao watapambana na Singida Black Stars mnamo tarehe 29 na 30 Oktoba 2025.
Ratiba hii imepangwa kwa kuzingatia kalenda ya FIFA, michuano ya kimataifa pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho, ili kuhakikisha usawa na uratibu mzuri wa msimu mzima.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba Yamtambulisha Selemani Mwalimu Kutoka Wydad AC kwa Mkopo wa Mwaka
- Simba Kuivaa Gor Mahia ya Kenya Kwenye Kilele cha Simba Day
- Mshambuliaji Clement Mzize Asaini Kuendelea na Yanga Hadi 2027
- Opah Clement Atambulishwa Rasmi SD Eibar ya Hispania
- Yanga SC Kucheza Dhidi ya Bandari FC Siku ya Wiki ya Mwananchi
- Morocco Yatinga Fainali ya CHAN Baada ya Kuifunga Senegal kwa Penalti
- Madagascar Kukipiga Dhidi ya Morocco Fainali ya CHAN 2025
Leave a Reply