Madagascar Kukipiga Dhidi ya Morocco Fainali ya CHAN 2025
Leo hatua ya nusu fainali ya michuano ya CHAN 2025 imehitimishwa kwa mechi mbili za kusisimua zilizofanyika kwenye viwanja vya Afrika Mashariki. Katika mchezo wa kwanza, Madagascar iliandika historia kwa kufuzu fainali kwa mara ya kwanza baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudan, bao ambalo lilipatikana kwenye dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa. Ushindi huu uliwapa Wamalagasi nafasi ya kipekee ya kuendeleza ndoto zao za kutwaa taji la CHAN.
Katika nusu fainali ya pili, Morocco ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Senegal ndani ya dakika 90 za kawaida. Mchezo huo ulilazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti ambapo Morocco walipata ushindi wa penalti 5-4 na kuweka wazi fainali ya kuvutia kati ya Madagascar na Morocco itakayochezwa Agosti 30, 2025, kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi, Kenya.
Safari ya Madagascar Kuelekea Fainali
Madagascar ilianza safari yake ya CHAN 2025 kwa uimara mkubwa. Katika nusu fainali dhidi ya Sudan, walicheza kwa tahadhari kubwa kipindi cha kwanza huku wakipiga mashuti sita, moja pekee likilenga lango. Sudan nao walipiga mashuti matatu, yote yakilenga lango lakini bila mafanikio ya kufunga.
Hali ilibadilika dakika ya 79 wakati kiungo wao Fenohasina Razafimaro alipoonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje, na hivyo kuacha Madagascar wakiwa pungufu. Hata hivyo, walionyesha uthabiti mkubwa na kuendelea kudhibiti mchezo hadi dakika za nyongeza.
Bao la ushindi lilifungwa dakika ya 116 na Toky Rakotondraibe akiunganisha pasi safi ya Randrianirina, na kupeleka mashabiki wa Madagascar kwenye furaha isiyoelezeka.
Morocco Yavua Ubingwa Senegal
Kwa upande mwingine, Morocco ilionyesha ubora wake kwa kuiondoa Senegal – mabingwa watetezi – kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1. Ushindi huu umeweka matumaini mapya kwa Morocco ambayo sasa inalenga kutwaa ubingwa wa CHAN 2025 kwa kishindo.
Fainali Inayotarajiwa: Madagascar vs Morocco
Mchuano wa fainali kati ya Madagascar na Morocco unatarajiwa kuwa wa kihistoria. Madagascar inatafuta taji lao la kwanza la CHAN, huku Morocco ikilenga kuongeza heshima yake katika michuano hii mikubwa ya wachezaji wa ligi za ndani.
Fainali hii itapigwa Agosti 30, 2025 kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi, na inatarajiwa kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki kutoka pande zote za Afrika.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba SC Yasogeza Tarehe ya Uzinduzi wa Jezi Mpya 2025/2026
- Viingilio Simba Day 2025
- Ligi Kuu Zanzibar ZPL 2025/2026 kuanza Septemba 20
- Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 | Picha za Jezi Mpya za Yanga
- Bei ya Jezi Mpya za Yanga 2025/2026
- Matokeo ya Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
- Kikosi cha Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
- Cv ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026
- Wafungaji Bora CHAN 2025
Leave a Reply