Magoli ya Stephan Aziz NBC 2023/2024: Orodha Kamili ya Timu Alizozifunga
Msimu wa 2023/2024 wa Ligi Kuu ya NBC utabaki kwenye kumbukumbu za mashabiki wengi wa Young Africans (“Yanga”) kama msimu wa kihistoria. Sio tu kwa sababu ya kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo, bali pia kwa sababu ya uwepo wa wachezaji wao ambao wamekua na muendelezo wa kua na ubora mkubwa. Miongoni mwa nyota waliong’ara zaidi katika msimu wa 2023/2024 ni Stephan Aziz Ki.
Kiungo huyu mwenye uwezo wa hali ya juu aliibuka kuwa mchezaji muhimu zaidi katika kikosi cha Yanga, akiwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu hiyo. Uwezo wake wa kufunga magoli ulikuwa wa kipekee, akitikisa nyavu mara 21 katika Ligi Kuu pekee. Magoli haya hayakuwa ya kawaida tu, bali yalikuwa magoli muhimu yaliyoipa Yanga alama tatu muhimu katika michezo mingi.
Yanga ilimaliza msimu kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, ikiwa na pointi 80. Kiasi hiki cha pointi kilipatikana kutokana na ushindi wa mechi nyingi, huku wakifunga jumla ya magoli 71 na kuruhusu kufungwa magoli 14 pekee. Mchango wa Aziz Ki katika takwimu hizi hauwezi kupuuzwa, kwani magoli yake 21 yalichangia takriban 30% ya magoli yote ya Yanga msimu huo.
Makala haya yanakuletea orodha kamili ya timu zote alizozifunga Aziz Ki katika msimu huu wa kihistoria. Ni safari ya kusisimua inayoonyesha ubora na umahiri wa mchezaji huyu aliyeibuka kuwa shujaa wa Jangwani.
Magoli ya Stephan Aziz NBC 2023/2024: Orodha Kamili ya Timu Alizozifunga
Sn | Timu Iliyofungwa | Idadi Ya Magoli |
1 | Prisons | 3 |
2 | Tabora | 1 |
3 | Dodoma Jiji | 2 |
4 | Simba SC | 1 |
5 | Fountain Gate | 1 |
6 | Geita Gold | 1 |
7 | Ihefu | 1 |
8 | Namungo | 1 |
9 | Tabora United | 1 |
10 | Mtibwa Sugar | 2 |
11 | Simba SC | 1 |
12 | Azam Fc | 3 |
13 | Geita Gold | 1 |
14 | JKT | 1 |
15 | KMC FC | 1 |
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Hizi Apa Takwimu za Stephane Aziz Ki na Feisal Salum 2023/2024
- Fei Toto na Aziz KI: Kinyanganyiro cha Mfungaji Bora Ligi Kuu Kushika Moto
- Wachezaji Wanaolipwa Pesa Nyingi Yanga 2024/2025
- Fei Toto Aweka Wazi Nia ya Kuvaa Jezi Nyekundu ya Al Ahly
- Mishahara ya Wachezaji wa Yanga sc 2024
- Timu za Tanzania Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Picha Za Parade ya Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24
Weka Komenti