Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 Mujibu wa Sheria
Dodoma, Mei 27, 2025 – Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo limetangaza rasmi majina ya wanafunzi wa kidato cha sita waliohitimu mwaka 2025 waliotakiwa kujiunga na mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria. Mafunzo haya ni ya lazima kwa kundi hilo la vijana na yanatarajiwa kuanza katika kambi mbalimbali nchini kuanzia Mei 28 hadi Juni 8, 2025.
Tangazo hilo limetolewa na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Juma Mrai, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Rajabu Mabele. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vijana wote waliotajwa wanapaswa kuripoti katika makambi ya JKT waliopangiwa ndani ya muda uliopangwa ili kushiriki katika mafunzo hayo ya kisheria.
Makambi ya JKT Yaliyopangwa kwa Mafunzo ya Mujibu wa Sheria
Vijana waliochaguliwa wamegawanywa katika makambi yafuatayo:
- Kanda ya Kaskazini na Kati: Rwamkoma (Mara), Msange (Tabora), Mpwapwa na Makutopora (Dodoma).
- Kanda ya Mashariki: Ruvu na Kibiti (Pwani).
- Kanda ya Nyanda za Juu Kusini: Mafinga (Iringa), Mlale (Ruvuma).
- Kanda ya Kaskazini-Mashariki: Mpambo na Maramba (Tanga), Makuyuni na Orjolo (Arusha).
- Kanda ya Magharibi: Bulombora, Kanembwa na Mtabila (Kigoma), Itaka (Songwe), Luwa na Milundikwa (Rukwa).
- Kanda ya Kusini: Nachingwea (Lindi).
Kwa vijana wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities), wameratibiwa kuripoti katika Kambi ya Ruvu, iliyopo Mlandizi, mkoa wa Pwani, ambayo ina miundombinu rafiki kwa ajili ya kuhudumia kundi hilo maalum.
Vifaa Muhimu Kwa Washiriki wa Mafunzo
Jeshi la Kujenga Taifa limeelekeza kuwa kila kijana anapaswa kufika kambini akiwa na vifaa vifuatavyo:
- Bukta ya rangi ya bluu iliyokoza, yenye mpira kiunoni, mfuko mmoja wa nyuma, urefu wa magotini na isiyo na zipu.
- Fulana ya kijani.
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani na bluu.
- Shuka mbili za rangi ya bluu bahari.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi kali.
- Traki suti ya kijani au bluu.
- Nyaraka muhimu kama cheti cha kuzaliwa na vyeti vya kuhitimu kidato cha nne.
- Nauli ya kwenda na kurudi kutoka kambini.
Jinsi ya Kupata Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 Mujibu wa Sheria
Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa pamoja na kambi walizopangiwa na vifaa vinavyotakiwa imechapishwa kupitia tovuti rasmi ya JKT: www.jkt.mil.tz.
Bofya Hapa Kupakua Majina ya Waliochaguliwa JKT
Ili kuona jina na kambi husika, kijana anatakiwa kuingiza jina la shule aliyosoma pamoja na namba ya shule mbele ya jina hilo. Atakapoona maneno “waliochaguliwa,” anaweza kubofya ili kuona maelezo kamili ya jina lake, jina la kambi, mkoa na wilaya ambako mafunzo yatafanyika.
Dhamira ya Mafunzo na Maendeleo ya Miundombinu
Kwa mujibu wa Kanali Mrai, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amewakaribisha vijana wote waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka 2025 kujiunga na wenzao katika zoezi hili muhimu la kujenga uzalendo, stadi za kazi na maisha, pamoja na kuimarisha umoja wa kitaifa.
Akizungumza kuhusu bajeti ya mwaka 2025/26, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax alieleza kuwa Serikali imeboresha miundombinu ya makambi kwa lengo la kuhakikisha vijana wote waliohitimu kidato cha sita wanapata fursa ya kushiriki mafunzo hayo. Kulingana na taarifa hiyo, JKT sasa lina uwezo wa kupokea hadi vijana 60,000, ikilinganishwa na vijana 40,000 mwaka 2021.
Wahitimu wote wanakumbushwa kuwa kutofika kambini ndani ya muda uliopangwa kunaweza kuathiri ushiriki wao rasmi katika zoezi hili la mafunzo ya kisheria. Aidha, ni muhimu kuhakikisha vifaa vyote vinavyotakiwa vinaandaliwa mapema kabla ya tarehe ya kuripoti.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ni Lini TAMISEMI Itatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026?
- Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
- Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)
- Waliochaguliwa Kidato cha Tano Mkoa wa Dodoma 2025/2026
- Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano Dar es Salaam 2025/2026
- Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2025/2026
Leave a Reply