Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Kusimamia Uchaguzi 2025 Dodoma
Kama wewe ni miongoni mwa maelfu ya waombaji waliokuwa wakisubiri matokeo ya usaili wa nafasi za muda za kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika Jiji la Dodoma, taarifa rasmi sasa imetolewa.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba ametangaza rasmi majina ya walioitwa kwenye mafunzo kusimamia uchaguzi 2025 Dodoma, kwa wale wote waliofaulu mafanikio katika usaili uliofanyika tarehe 11 Oktoba 2025.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mafunzo haya ni ya lazima kwa wote walioteuliwa, na yanahusisha makarani waongozaji wapiga kura pamoja na wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura. Mafunzo haya ni sehemu muhimu katika maandalizi ya uchaguzi, yakilenga kuwajengea uelewa na ujuzi wa kiutendaji watakaohusika kuhakikisha mchakato wa kupiga kura unafanyika kwa uwazi, uadilifu, na ufanisi.
Ratiba ya Mafunzo kwa Walioitwa Kusimamia Uchaguzi 2025 Dodoma
Kwa mujibu wa tangazo rasmi lililotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo hayo, mafunzo yamepangwa kufanyika kama ifuatavyo:
Makarani Waongozaji wa Wapiga Kura
- Tarehe ya Mafunzo: 25 Oktoba 2025
- Maeneo ya Mafunzo: Ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gaspar (Jimbo la Dodoma Mjini) & Ukumbi wa Mtumba Complex (Jimbo la Mtumba)
Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura
- Tarehe za Mafunzo: 26 – 27 Oktoba 2025
- Maeneo ya Mafunzo: Mtumba Complex, Shule ya Sekondari Dkt. Samia Lyumbu, Four Points Kisasa & Shule ya Msingi St. Gaspar Miyuji
Mafunzo yote yamepangwa kuanza saa 1:30 asubuhi katika kumbi zote zilizotajwa. Washiriki wote wametakiwa kufika kwa wakati bila kukosa, ili kuepuka kupoteza nafasi yao ya kushiriki katika mchakato wa usimamizi wa uchaguzi.
Umuhimu wa Mafunzo Haya
Mafunzo haya yanachukuliwa kuwa hatua muhimu kabla ya siku ya uchaguzi. Watendaji watakaoshiriki wanatarajiwa kujifunza taratibu sahihi za kusimamia wapiga kura, kuhakikisha usahihi katika orodha za wapiga kura, na kudumisha misingi ya haki na uwazi katika vituo vyao vya kazi. Kupitia mafunzo haya, Msimamizi wa Uchaguzi anatarajia kujenga timu imara ya wasimamizi wenye uelewa wa kutosha kuhusu majukumu yao na kanuni za uchaguzi. Hivyo, ni wajibu wa kila aliyeitwa kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika mafunzo haya ili kuchangia katika kufanikisha uchaguzi wa amani na uwazi jijini Dodoma.
Pakua Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Kusimamia Uchaguzi 2025 Dodoma Pdf
Kwa urahisi wa kupata taarifa kamili, waombaji wote wanaweza kupakua orodha rasmi ya majina na matangazo husika kupitia viungo vya nyaraka (PDF) zilizotolewa na Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba.
Bonyeza viungo vifuatavyo ili kupakua majina kamili:
- Tangazo La Kuitwa Kwenye Mafunzo Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi Na Makarani Jimbo La Dodoma Mjini Na Mtumba.Pdf
- Orodha Ya Majina Wasimamizi Na Wasimamizi Wasaidizi Na Makarani Wa Vituo Vya Kupigia Kura Kwa Ajili Ya Mafunzo Jimbo La Dodoma Mjini.Pdf
- Orodha Ya Majina Ya Wasimamizi Na Wasimamizi Wasaidizi Wa Vituo Vya Kupigia Kuwa Kwa Ajili Ya Mafunzo Jimbo La Mtumba.Pdf
- Orodha – Wasimamizi Wa Akiba Wa Uchaguzi Kwa Ajili Ya Mafunzo.Pdf
- Orodha – Makarani Akiba Kwa Ajili Ya Mafunzo.Pdf
Mapendekezo ya Mhariri:
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025
- Nafasi Mpya 10026 za Kazi Walimu MDAs & LGAs 2025
- Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal
- Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025
- Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo ya Kusimamia Uchaguzi INEC 2025 Mkoa wa Singida
- Ajira Mpya za Walimu MDAs & LGAs 2025: Nafasi 3018 za Mwalimu Daraja la IIIA Zatangazwa
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025 Kigamboni









Leave a Reply