Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo ya Kusimamia Uchaguzi INEC 2025 Mkoa wa Singida
Kwa ajili ya maandalizi ya uendeshaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ilongero, mkoani Singida, ametangaza rasmi majina ya walioitwa kwenye mafunzo ya kusimamia uchaguzi chini ya uongozi wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). Tangazo hili limezingatia masharti ya kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024, kikisomwa kwa pamoja na kanuni ya 11 ya Kanuni za Uchaguzi wa mwaka 2025.
Mafunzo haya yameandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo Wasimamizi wa Vituo, Wasimamizi Wasaidizi, na Makarani wa Vituo vya Kupigia Kura, ambao wamechaguliwa kushiriki katika zoezi la kusimamia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Ratiba ya Mafunzo ya Kusimamia Uchaguzi INEC 2025 Mkoa wa Singida
Kwa mujibu wa tangazo rasmi la Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ilongero, mafunzo yatafanyika katika ngazi ya Tarafa, yakianza saa 1:00 asubuhi kwa siku zilizopangwa kama ifuatavyo:
- Tarehe 25 Oktoba, 2025 – Mafunzo maalum kwa Makarani waongozi wa vituo vya kupigia kura.
- Eneo: Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilongero, Mkoa wa Singida.
- Tarehe 26 – 27 Oktoba, 2025 – mafunzo kwa Wasimamizi wa vituo na wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura katika kumbi zifuatazo;
Lengo Kuu la Mafunzo
Mafunzo haya yanatolewa ili kuhakikisha kuwa kila mtendaji aliyechaguliwa anapata uelewa sahihi kuhusu:
- Taratibu za kusimamia uchaguzi kwa uwazi na uadilifu.
- Uendeshaji wa vituo vya kupigia kura kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.
- Usimamizi sahihi wa vifaa na nyaraka za uchaguzi.
- Uhakikisho wa usalama na uwazi wakati wa kuhesabu na kutangaza matokeo.
INEC inalenga kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 unafanyika kwa amani, uwazi, na ufanisi, kwa kuandaa watendaji walio na maarifa ya kutosha katika utekelezaji wa majukumu yao.
Bofya Hapa Kupakua Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Kusimamia Uchaguzi INEC 2025 Mkoa wa Singida
Mapendekezo ya Mhariri:
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025 Kigamboni
- Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025
- Mfano Wa Barua Ya Kuomba Kazi Mwalimu Daraja La IIIA
- Mfano Wa Barua Ya Kuomba Kazi Afisa Muuguzi Msaidizi II
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili INEC 2025
- Posho na Malipo ya Wasimamizi wa Uchaguzi 2025
Leave a Reply