Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026

Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026 | Shule walizopangiwa form one 2026 (Shule walizopangiwa kidato cha kwanza 2026) | Uchaguzi wa Kidato cha Kwanza 2026 | Shule walizopangiwa Darasa la saba

Baada ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kutangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025 (PSLE) tarehe 5 Novemba 2025 jijini Dar es Salaam, kupitia kwa Katibu Mtendaji Prof. Said A. Mohamed, hatua inayofuata imekuwa kusubiri taarifa za upangaji wa wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2026. Zaidi ya watahiniwa 937,581 waliofaulu sasa wanangojea kujua shule watakazopangiwa, suala ambalo kwa miaka mingi limekuwa likifuatiliwa kwa umakini mkubwa na wazazi, walezi na jamii kwa ujumla.

Uteuzi huu, unaoratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na NECTA, huainisha mgawanyo wa wanafunzi katika shule za bweni na kutwa za serikali ikiwemo shule za kitaifa na zile za mfano.

Mchakato huu ni muhimu kwa sababu unaweka msisitizo kwenye usawa wa fursa, hasa kwa wanafunzi wanaotoka katika mazingira mbalimbali, imewahi kufafanuliwa katika moja ya taarifa za TAMISEMI kuhusu uchaguzi wa wanafunzi.

Kwa mzazi, mlezi au mwanafunzi anayetaka kufahamu hatua kamili za kuangalia Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026, hapa chini tumekusanya mwongozo uliofafanuliwa kwa umakini ukieleza hatua, sifa za uteuzi na namna ya kupata orodha kamili ya majina kupitia chanzo rasmi.

Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026

Serikali ya Tanzania kupitia Tamisemi na NECTA, kwa kushirikiana na Baraza la mitihani Tanzania (NECTA), hutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza miezi michache baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE). Huu ni mchakato muhimu na unaosubiriwa kwa hamu na wazazi, wanafunzi, na jamii kwa ujumla. Hapa tunakuletea hatua rahisi za kufuata ili uweze kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2025.

Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026

Kwa kawaida, baada ya TAMISEMI kukamilisha upangaji wa wanafunzi, taarifa hupakiwa kwenye tovuti za serikali kwa matumizi ya wananchi. Ufuatao ni mwongozo wa moja kwa moja:

1. Fungua tovuti ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz)

Tovuti ya TAMISEMI ndio chanzo kikuu cha taarifa za matokeo na uteuzi wa wanafunzi. Baada ya kufungua tovuti ya TAMISEMI, shuka hadi chini sehemu yenye “Matangazo Muhimu”. Hapa ndipo taarifa kuhusu uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza huwekwa

Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026

2. Chagua kipengele cha orodha ya uteuzi

Kwa kawaida, kipengele hiki huwekwa kwenye ukurasa wa mbele ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa. Kinaongoza moja kwa moja kwenye orodha ya mikoa yote ya Tanzania Bara.

Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025

3. Chagua Mkoa → Wilaya

Baada ya kuchagua mkoa, utaelekezwa kwenye orodha ya wilaya zote zinazohusika. Chagua wilaya ya shule ya msingi ya mwanafunzi.

4. Chagua shule ya msingi

Sehemu hii ina majina ya shule zote za msingi zilizopo ndani ya wilaya. Ukibofya shule husika, utaona majina ya wanafunzi wote waliopangiwa, pamoja na taarifa za shule walizoelekezwa kujiunga nazo.

Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025

5. Pakua hati ya PDF

Kila shule imewekewa hati ya PDF kwa urahisi wa kupakua na kutunza taarifa. Hii inawasaidia wazazi na wanafunzi kuwa na kumbukumbu ya kudumu.

Ni Lini Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026 Yatatangazwa?

Hadi sasa, TAMISEMI haijatoa tamko rasmi kuhusu tarehe halisi ya kutangazwa kwa orodha ya wanafunzi watakaopangiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2026. Hata hivyo, kwa kuzingatia mfuatano wa matukio katika ratiba ya elimu pamoja na mwenendo wa miaka iliyopita, utoaji wa majina haya kwa kawaida hufanyika baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa matokeo ya PSLE na uhakiki wa nafasi za shule. Kutokana na utaratibu huo, inatarajiwa kuwa tangazo rasmi la Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026 litatolewa mwezi Desemba 2026, mara tu taratibu za upangaji zitakapokamilika.

Sifa Zinazotumika Kuwachagua Wanafunzi Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2026

Katika mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na Kidato cha Kwanza 2026, TAMISEMI huzingatia kiwango cha ufaulu cha mwanafunzi katika Mtihani wa Darasa la Saba, ambapo alama kati ya 121 na 300 ndizo zinazohitajika kama kigezo cha msingi cha uteuzi.

Wanafunzi wenye alama za juu hupata nafasi katika shule zenye hadhi ya kitaifa na zile za ufundi, huku nafasi katika shule za bweni za kawaida zikielekezwa zaidi kwa wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu, maeneo ya vijijini, au familia zenye kipato cha chini.

Aidha, serikali hutoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu, changamoto za kiafya au wale wanaolelewa katika vituo vya watoto yatima, ili kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa elimu kwa wote.

Kwa wale wanaosubiri tangazo la Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026, ni muhimu kufuatilia karibu taarifa kutoka TAMISEMI na NECTA kupitia tovuti zao. Mchakato wa uteuzi umeandaliwa ili kuhakikisha usawa, uwazi na nafasi kwa wanafunzi wote waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba 2025. Kwa kufuata hatua zilizoainishwa, wazazi na wanafunzi wanaweza kupata majina hayo kwa urahisi na haraka, bila mkanganyiko.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  2. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE)
  3. Kidato cha Nne Kuanza Mitihani ya Taifa Kesho November 17 2025
  4. NECTA Standard Seven Results 2025 Released: 81.8% of Candidates Pass the PSLE Examination
  5. Tarehe Mpya za Kufunguliwa Vyuo 2025/2026 Zatangazwa na Wizara ya Elimu
  6. NECTA Yatangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2025 – Asilimia 81.80 Wamefaulu Nchini
  7. Mambo 5 ya Muhimu Kujua Wakati Wa Kusubiri Kutangazwa kwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo