Makundi ya Kombe La Dunia 2026
Michuano ya Kombe la Dunia 2026 inatarajiwa kuwa ya kipekee na ya kihistoria, ikiwa ni mara ya kwanza kushirikisha timu 48 badala ya 32 zilizoshiriki katika toleo lililopita. Mashindano haya makubwa zaidi duniani yatafanyika kuanzia tarehe 11 Juni hadi 19 Julai, yakihusisha nchi tatu wenyeji: Marekani, Canada na Mexico.
Baada ya mchakato mrefu wa kufuzu ulioanza Septemba 2023, hatimaye timu zote 48 zimethibitishwa kushiriki. Timu za mwisho kufuzu ni DR Congo na Iraq, zikikamilisha orodha ya washiriki wa mashindano haya ya kihistoria
Mfumo Mpya wa Kombe la Dunia 2026
Kombe la Dunia Msimu huu wa 2026 linakuja na mabadiliko makubwa katika mfumo wa mashindano:
- Jumla ya timu 48 zitashiriki
- Makundi 12, kila kundi lina timu 4
- Jumla ya mechi 104 zitachezwa
- Mashindano yatafanyika kwa siku 39
- Mechi zitachezwa katika miji 16
Timu mbili bora kutoka kila kundi pamoja na timu nane bora zilizoshika nafasi ya tatu zitafuzu hatua ya mtoano (Round of 32).
Fainali itachezwa tarehe 19 Julai katika uwanja wa MetLife Stadium, New Jersey
Makundi ya Kombe La Dunia 2026
Haya ndiyo makundi rasmi ya Kombe la Dunia 2026:
Kundi A
- Mexico
- South Africa
- South Korea
- Czech Republic
Kundi B
- Canada
- Bosnia-Herzegovina
- Qatar
- Switzerland
Kundi C
- Brazil
- Morocco
- Haiti
- Scotland
Kundi D
- United States
- Paraguay
- Australia
- Turkey
Kundi E
- Germany
- Curaçao
- Ivory Coast
- Ecuador
Kundi F
- Netherlands
- Japan
- Tunisia
- Sweden
Kundi G
- Belgium
- Egypt
- Iran
- New Zealand
Kundi H
- Spain
- Cape Verde
- Saudi Arabia
- Uruguay
Kundi I
- France
- Senegal
- Iraq
- Norway
Kundi J
- Argentina
- Algeria
- Austria
- Jordan
Kundi K
- Portugal
- DR Congo
- Uzbekistan
- Colombia
Kundi L
- England
- Croatia
- Ghana
- Panama
Makundi haya yanaonyesha ushindani mkali, hasa katika makundi yenye timu kubwa kama Brazil, Argentina, Spain, na France.
Timu Zinazotajwa Kuwa na Nafasi Kubwa ya Kuchukua Kombe
Kwa mujibu wa mwenendo wa kufuzu:
Spain wanaingia kama mabingwa wa Ulaya na wana kikosi chenye vipaji vingi
England wana rekodi nzuri ya kufuzu bila kufungwa
France wana safu kali ya ushambuliaji
Argentina, mabingwa watetezi, wanaendelea kuwa na nguvu kubwa
Brazil, licha ya changamoto za kufuzu, bado ni tishio kutokana na historia yao
Mashindano haya yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya timu.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply