Mamelodi Sundowns Bingwa Tena wa Ligi Kuu Afrika Kusini 2024/25

Mamelodi Sundowns Bingwa Tena wa Ligi Kuu Afrika Kusini 2024 25

Mamelodi Sundowns Bingwa Tena wa Ligi Kuu Afrika Kusini 2024/25

Mamelodi Sundowns wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) kwa msimu wa 2024/25 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chippa United katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Buffalo City. Kwa ushindi huu, Sundowns wamefikisha pointi 70 katika mechi 27 walizocheza, wakiacha pengo la pointi 15 dhidi ya Orlando Pirates waliopo nafasi ya pili kwa pointi 55 katika michezo 24.

Huu ni ubingwa wa nane mfululizo kwa Masandawana katika Ligi hiyo, na wa 17 kwa jumla tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Kwa mafanikio haya, Mamelodi Sundowns wamejikita rasmi kama klabu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya PSL, wakiwa wamewapiku wapinzani wao wa karibu – Kaizer Chiefs wenye mataji 13 na Orlando Pirates wenye mataji 9.

Mamelodi Sundowns Bingwa Tena wa Ligi Kuu Afrika Kusini 2024/25

Mchezo Dhidi ya Chippa United: Hatua ya Kufunga Historia

Katika mchezo huo wa kihistoria, Iqraam Rayners aliwapa uongozi Mamelodi Sundowns kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 10. Bao hilo lilikuwa la 14 kwa mchezaji huyo msimu huu. Kipindi cha pili kilishuhudia Arthur Sales akiingia na kuongeza mabao mawili, akifunga dakika ya 69 na dakika ya 89, kufuatia makosa ya kipa wa Chippa United, Darren Johnson.

Ushindi huu umeandikwa chini ya Kocha Miguel Cardoso, ambaye ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutoka Ureno kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Hii inaifanya Mamelodi kuwa klabu ya kipekee ambayo imetwaa mataji nane mfululizo chini ya makocha wanne tofauti:

  • Pitso Mosimane (mataji 3),
  • Rhulani Mokwena (mataji 4),
  • Miguel Cardoso (taji 1).

Kocha Cardoso amesema kuwa mafanikio haya ni matokeo ya bidii na malengo ya muda mrefu. Alieleza kuwa, “Tunapaswa kusherehekea kwa mbwembwe kwa sababu kuna rekodi tumezivunja, nafikiri historia imeandikwa. Tamaa ni jambo muhimu katika mchezo wa soka…”

Miongoni mwa wachezaji waliowahi kung’ara katika historia ya klabu hiyo ni Hlompho Kekana, aliyestaafu mwaka 2021, akiwa na mataji 6 ya ligi akiwa nahodha na kiungo wa kati.

Kwa upande mwingine, baadhi ya wachezaji wa sasa wa kikosi cha Mamelodi Sundowns wameonja ubingwa huu kwa mara ya kwanza. Hawa ni pamoja na:

  • Lucas Suarez
  • Matias Esquivel
  • Iqraam Rayners
  • Abram Mashele – kinda kutoka akademi ya klabu ambaye amepewa nafasi kikosi cha wakubwa.

Safari Iliyosalia: Ndoto ya Ubingwa wa Afrika

Baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu, Mamelodi Sundowns sasa wanatazama mbele kwa matumaini ya kuongeza taji lingine. Watashuka dimbani kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri. Mchezo wa kwanza utafanyika nyumbani Mei 24, huku wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa Juni 1, 2025.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Beki wa Taifa Stars Haji Mnoga Kubaki Salford City kwa Mwaka Mwingine
  2. Fountain Gate Njia Panda Baada ya Kichapo Dhidi ya JKT
  3. Timu Zilizoshuka Daraja Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
  4. Matokeo ya Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025
  5. Dickson Ambundo Ajiweka Sokoni Huku Fountain Gate Ikipambana Kubaki Ligi Kuu
  6. Yanga Yaanza Kutega Mitego ya Kumnasa Marcel Koller, Aliyekuwa Kocha Ahly
  7. Simba Yaendelea Kugawa Dozi Kwa Kila Anayekutana Naye Ligi Kuu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo