Man City Yaibuka na Ushindi wa 3-0 Dhidi ya Manchester United

Man City Yaibuka na Ushindi wa 3-0 Dhidi ya Manchester United

Manchester United imekubali kichapo cha pili cha msimu baada ya kulala 3-0 dhidi ya Manchester City katika dimba la Etihad kwenye Manchester Derby, huku wapinzani wao wakirejea kwenye hali ya ushindi baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu England (EPL). Ushindi huu umeipa nguvu mpya City na kuongeza shinikizo kwa United ambao wameanza msimu kwa matokeo duni.

Man City Yaibuka na Ushindi wa 3-0 Dhidi ya Manchester United

Mchezo ulivyokuwa

Katika pambano hilo la kukumbukwa, Manchester City iliitawala michezo kwa ufanisi mkubwa, ikionesha uimara wao hususan katika safu ya ushambuliaji. Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 18 kupitia kichwa cha Phil Foden, baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Jeremy Doku, ambaye mara kadhaa aliisumbua ngome ya Manchester United.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa bao moja pekee, lakini mara tu baada ya kipindi cha pili kuanza, City waliongeza kasi. Dakika ya 53, Erling Haaland aliongeza bao la pili, tena akimalizia mpira wa Doku. Mshambuliaji huyo wa Norway hakusita kuweka historia zaidi dakika ya 68 alipofunga bao la tatu kwa pasi safi kutoka kwa Bernardo Silva na kuhitimisha karamu ya mabao kwa wenyeji.

Taarifa Muhimu za Takwimu

Ushindi huu wa Man City kwa 3-0 dhidi ya Manchester United unaongeza rekodi nzuri ya City katika mechi tano za hivi karibuni za EPL dhidi ya mahasimu wao. Wameibuka na ushindi mara tatu, sare moja na kipigo mara moja pekee.

Kwa upande wa Haaland, mabao yake mawili yamemuweka kwenye orodha ya wachezaji wachache waliowahi kufunga mabao 50 katika michezo 50 ya nyumbani ya EPL. Kihistoria, ni Alan Shearer pekee aliyewahi kufanikisha rekodi hiyo mapema zaidi, kwa kufunga mabao 50 ndani ya michezo 47.

Msimamo wa Ligi Kuu England Baada ya Mechi

Matokeo haya yameifanya Manchester City kufikisha pointi sita na kupanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa EPL. Wakati huo huo, Manchester United imeendelea kusalia na pointi nne pekee na kushuka hadi nafasi ya 14.

Kwa United, huu ni mwanzo mbaya zaidi wa msimu tangu mwaka 1992/1993, ambapo walipata pointi chache katika michezo minne ya kwanza sawa na hali waliyonayo sasa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kelvin John Aendeleza Moto Baada ya Kuifungia Aalborg Goli 2 Wakiilaza Middelfart 4-0
  2. Msimamo Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga 2025/2026
  3. Juventus Yaicharaza Inter Milan 4-3 Ligi Kuu Italia
  4. Singida BS Yatinga Fainali ya CECAFA Kagame Cup Baada ya Kuifunga KMC 2-0
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo