Mashujaa vs Azam Leo 29/09/2024 Saa Ngapi?
Leo, tarehe 29 Septemba 2024, mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajia kushuhudia mechi kali kati ya Mashujaa FC na Azam FC. Mchezo huu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2024/2025 unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, na utaanza rasmi saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Mashujaa FC, ambao wameanza msimu huu kwa kiwango cha kuvutia, wana pointi nane baada ya mechi nne. Timu hii imefanikiwa kushinda mara mbili na kutoka sare mara mbili, huku wakifunga mabao manne na kuruhusu mabao mawili pekee. Mashujaa wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Pamba FC katika mechi yao ya mwisho.
Kwa upande mwingine, Azam FC wana pointi nane pia, lakini wao wamecheza mechi tano. Wakiwa na rekodi ya kushinda mara mbili, kutoka sare mara mbili, na kupoteza mchezo mmoja, Azam wanalenga kujiondoa kwenye hali ya kutokuridhisha baada ya kupoteza mechi yao ya mwisho kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC. Katika mechi za msimu uliopita, Azam walishinda 3-0 dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, huku mchezo wa pili ukimalizika kwa sare ya 0-0.
Wachezaji wa Kutazamiwa
Katika pambano hili, wachezaji kadhaa wamejipambanua kama nguzo muhimu kwa timu zao. Kwa upande wa Mashujaa FC, Crispin Ngushi na David Ulomi wamekuwa katika hali nzuri, kila mmoja akiwa amefunga mabao mawili hadi sasa msimu huu. Wachezaji hawa watakuwa nguzo muhimu kwa Mashujaa wanapojaribu kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Azam FC.
Kwa Azam FC, mchezaji hatari zaidi ni Nassor Saadun, ambaye tayari amefunga mabao mawili msimu huu. Mashujaa watahitaji kumchunga sana mchezaji huyu ili kudhibiti mashambulizi ya Azam. Kocha wa Mashujaa, Mohammed Abdalah ‘Baresi’, ameonyesha matumaini makubwa huku akiwataka wachezaji wake kujiandaa kwa mechi ngumu licha ya matokeo mabaya ya Azam katika mechi yao iliyopita.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti