Matokeo Kagera Sugar Vs Yanga Leo 29/08/2024 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Kagera Sugar
Bukoba, 29 Agosti 2024 – Leo Mji wa Bukoba utashuhudia mchuano mkali kati ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, na wenyeji wao Kagera Sugar katika dimba la Kaitaba.
Mchezo huu unatajwa kuwa muhimu kwa pande zote mbili, huku Yanga ikisaka ushindi wa kuanza msimu kwa mafanikio, na Kagera Sugar ikitafuta kurekebisha makosa baada ya kupoteza mechi ya awali dhidi ya Singida Black Stars. Mechi hii imepangwa kuanza majira ya saa 11 jioni na itaoneshwa mubashara kupitia kisimbuzi cha Azam Tv.
Yanga SC inashuka dimbani leo ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya Kagera Sugar. Katika mechi kumi za mwisho walizokutana kwenye uwanja wa Kaitaba, Yanga imeshinda mara nane, sare moja, na kupoteza mara moja tu.
Mabao 16 yamefungwa na Yanga katika mechi hizi, huku wakiwa wamezuia Kagera kufunga katika mechi saba kati ya hizo. Hii inaonesha ni jinsi gani Yanga imekuwa na ubora mkubwa inapocheza ugenini dhidi ya Kagera.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, anafahamu umuhimu wa mechi hii, hasa baada ya kuanza msimu kwa kishindo kwa kubeba Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na Azam, pamoja na kuibuka na ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 10-0 dhidi ya Vital’O ya Burundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Huu ni mwanzo mzuri kwa Yanga, na Gamondi anatarajia kuendeleza moto huo katika Ligi Kuu.
Gamondi amesema, “Tunahitaji kufikiria kuhusu sasa. Msimu uliopita tulipata matokeo yasiyokuwa mazuri hapa Kaitaba, lakini sasa hali ni tofauti. Tuko tayari kwa vita, ingawa tunajua uwanja ni mgumu.” Maneno haya yanaakisi nia ya Yanga kutetea ubingwa wao kwa mara ya nne mfululizo.
Kagera Sugar, chini ya kocha Paul Nkata, wanaingia katika mechi hii wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Singida Black Stars. Nkata ana matumaini makubwa ya kurekebisha makosa na kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa leo. Wachezaji wazoefu kama Obrey Chirwa, Nassor Kapama, na Cleophas Mkandala wanatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa Kagera katika kujaribu kuwabana Yanga.
Kocha Nkata amesema, “Tunajua Yanga ni timu nzuri, lakini tunahitaji kucheza kwa umakini na kujituma zaidi ya asilimia 200. Malengo yetu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika uwanja wetu wa nyumbani.”
Matokeo Kagera Sugar Vs Yanga Leo 29/08/2024
Kagara Sugar | 0-2 | Yanga Sc |
|
- 🏆 #NBCPremierLeague
- ⚽️ Kagera Sugar🆚Young Africans SC
- 📆 29.08.2024
- 🏟 Kaitaba
- 🕖 5:00PM
Angalia Hapa Kikosi cha Yanga Vs Kagera Sugar Leo 29/08/2024
Rekodi na Takwimu Muhimu
Katika misimu kumi iliyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kagera na Yanga zimekutana mara 20, ambapo Yanga imeshinda mara 16, sare mbili, na Kagera kushinda mara mbili tu. Kwa ujumla, Yanga imefunga mabao 41 dhidi ya Kagera katika kipindi hicho, huku Kagera wakifunga mabao 16 pekee.
Mechi ya mwisho kati ya timu hizi kwenye uwanja wa Kaitaba ilimalizika kwa sare ya 0-0, lakini Yanga ina kumbukumbu ya ushindi mkubwa wa 6-2 dhidi ya Kagera katika uwanja huu mwaka 2016. Hivyo, mashabiki wa Yanga wanatarajia kuona timu yao ikiendeleza rekodi nzuri na kurudi nyumbani na alama tatu.
Maneno ya Nahodha na Wachezaji wa Yanga
Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amewatoa hofu mashabiki kwa kusema, “Tunafahamu kuwa mashabiki wetu wanatoka mbali kuja kufuata furaha. Tunawahakikishia watarudi nyumbani wakiwa na furaha.”
Kwa upande wake, Nickson Kibabage, beki wa Yanga, ameongeza, “Mchezo uliopita katika uwanja huu hatukupata matokeo mazuri. Najua wachezaji wenzangu wanalitambua hilo. Bahati nzuri ni kwamba tumeshajiandaa vya kutosha kwa mchezo wa leo.”
Kocha Miguel Gamondi alisisitiza umuhimu wa alama tatu, akisema, “Huu ni mwanzo wa msimu, na tumewaeleza wachezaji wetu nini mashabiki wanahitaji. Jambo la kwanza ni alama tatu. Nafahamu mashabiki wetu wanatamani kweli tufunge magoli mengi, lakini kwetu sisi jambo la kwanza ni alama tatu.”
Hitimisho: Je, Yanga Itaendeleza Ubabe?
Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajia mchezo mkali na wa kuvutia kati ya Kagera Sugar na Yanga leo. Je, Yanga itaendeleza ubabe wake dhidi ya Kagera, au Kagera watafanya mabadiliko na kupata matokeo mazuri mbele ya mashabiki wao? Majibu yatapatikana baada ya kipenga cha mwisho. Endelea kufuatilia matokeo ya mechi hii hapa kwa updates za papo kwa papo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- RATIBA ya Mechi za Leo 29 August 2024
- Nyota Wawili Yanga Kuikosa Kagera Sugar
- Mabadiliko ya Ratiba Mechi ya Kagera Sugar vs Yanga
- JKT Tanzania na Azam FC Wagawana Pointi Mchezo wa Kwanza wa Ligi
- Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
- Timu zinazoshiriki African Football League AFL 2024/2025
Weka Komenti