Matokeo Simba Vs Al Adalah FC Leo (29/07/2024)- Mechi ya Kirafiki
Leo, Jumatatu tarehe 29 Julai 2024, klabu bingwa ya soka Tanzania, Simba Sports Club, itarejea uwanjani kucheza mchezo wao wa tatu wa kirafiki dhidi ya Al Adalah FC kutoka Saudi Arabia. Mechi hii inajumuishwa katika ratiba ya maandalizi ya Simba kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa msimu wa 2024/2025.
Mtanange huu mkali unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja mpya wa Suez Canal nchini Misri, kuanzia saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Kocha Mkuu wa Simba, pamoja na benchi lake la ufundi, wametumia mechi mbili zilizopita za kirafiki kujaribu mbinu mbalimbali za uchezaji na kuwapima wachezaji wapya waliosajiliwa hivi karibuni. Mchezo dhidi ya Al Adalah FC unatarajiwa kuwa kipimo kingine muhimu katika kutathmini uwezo wa kikosi kuelekea msimu mpya.
Simba SC: Kambini Kwenye Maandalizi ya Msimu Mpya
Simba SC, timu maarufu kutoka Tanzania, imekuwa katika kambi ya maandalizi nchini Misri ambapo wamecheza michezo miwili ya kirafiki hadi sasa. Katika michezo hii, wekundu wa Msimbazi wameonyesha kiwango cha juu na umoja wa timu.
Mchezo wa Kwanza: Simba SC ilikabiliana na El-Qanah, ambapo walionyesha uwezo wao wa kipekee kwa kushinda 3-0. Wachezaji wa Simba wanatumia mechi hizi za kirafiki kuonyesha kiwango chao cha juu na kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Mchezo wa Pili: Katika mchezo mwingine, Simba SC ilicheza dhidi ya Telecom Egypt na kushinda 2-1. Ushindi huu ulionyesha namna timu inavyojiandaa kwa umakini kwa ajili ya msimu ujao.
Al Adalah FC: Changamoto Kubwa kwa Simba SC
Katika mchezo wa leo, Simba SC itakutana na Al Adalah FC, timu kutoka Saudi Arabia inayoshiriki katika Ligi ya Daraja la Kwanza. Ingawa Al Adalah FC inashiriki katika ligi ya daraja la kwanza, ina wachezaji wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kutosha. Timu hii imejipanga vyema na inatarajiwa kutoa changamoto kubwa zaidi kwa Simba SC kulinganisha na michezo miwili iliyopita. Hii ni fursa nzuri kwa Simba SC kujipima dhidi ya upinzani wenye nguvu na kuhakikisha maandalizi yao yanaenda vizuri kabla ya kuanza kwa msimu wa 2024/2025.
Matokeo Simba Vs Al Adalah FC Leo (29/07/2024)
Simba Sc | 2-1 FT | Al Adalah FC |
- Dakika ya 9 Mukwala anaipa Simba Goli la Kwanza
- Dakika ya 32, Mutale anaongeza Goli kwa Wekundu wa msimbazi
Angalia Hapa Kikosi Cha Simba Vs Al Adalah FC Leo (29/07/2024)
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Kucheza na Red Arrows Siku ya Yanga Day 2024
- Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo 28/07/2024 – Toyota Cup
- Aziz Ki Atawazwa Mchezaji Bora Fainali Toyota Cup 2024
- Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 – Toyota Cup
- Matokeo Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki
- Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki
- Hizi Apa Picha Za Jezi Mpya Ya Yanga Sc 2024/2025
- Hivi Apa Vituo Vya Kununua Tiketi Simba Day 2024
- Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu NBC 2023/2024: Hawa Ndio Wagombea
Weka Komenti