Matokeo Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Matokeo Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Jumatano, Oktoba 8, 2025, itashuka dimbani katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kwa mchezo wa kukamilisha safari ya kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa kukutana na Timu ya Taifa ya Zambia.

Stars inaingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi E ikiwa na alama 10, nyuma ya vinara Morocco wenye alama 21, ambao tayari wamefuzu moja kwa moja. Kwa upande wa Zambia, wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama 6 baada ya mechi kadhaa zenye ushindani mkubwa.

Katika mchezo wa awali kati ya timu hizo, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zambia, bao pekee likifungwa na Wazir Junior, ushindi uliowapa matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu kabla ya matokeo yasiyoridhisha dhidi ya Morocco, Congo na Niger.

Baada ya ushindi huo, Stars ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na Morocco, ikatoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Congo, na baadaye kupoteza 1-0 dhidi ya Niger, matokeo yaliyowapunguza nafasi za kucheza hatua ya mchujo.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano, vinara wa makundi tisa wanapita moja kwa moja kushiriki fainali, huku timu nne bora zilizoshindwa kumaliza vinara zikitarajiwa kucheza hatua ya mchujo kuanzia nusu fainali hadi fainali, ambapo mshindi ataungana na wawakilishi kutoka mabara mengine.

Kwa sasa, timu zenye nafasi nzuri ya kupenya kupitia mlango wa mchujo ni Gabon (alama 19), Madagascar na DR Congo (alama 16), pamoja na Burkina Faso, Cameroon, Namibia na Uganda (alama 15), hivyo matokeo ya michezo ya mwisho yataamua hatima yao.

Akizungumza kabla ya mchezo huu, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, alisisitiza kuwa maandalizi yamekamilika na wachezaji wako tayari kupambana hadi dakika ya mwisho.

“Haitakuwa mechi nyepesi hata kidogo kwa sababu Zambia ni miongoni mwa mataifa shindani. Hivi karibuni wamekuwa wakipitia kipindi kigumu, lakini hilo haliwezi kuondoa ubora wao. Tumejiandaa vya kutosha na naamini tutafanya vizuri na kuwapa burudani mashabiki wetu,” alisema Kocha Morocco.

Kwa upande wa Zambia, kiungo Clatous Chama aliwahimiza mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo akisema:

“Tanzania ni wapinzani wagumu, tumekuwa tunafahamiana kwa muda mrefu, kwa hiyo itakuwa mechi nzuri na yenye ushindani mkubwa,” alisema Chama.

Licha ya ushindi wa Taifa Stars katika mchezo wa mwisho ugenini, rekodi inaonyesha Tanzania imekuwa na wakati mgumu inapokutana na Zambia nyumbani. Katika mechi tano za kirafiki zilizopita, Stars imetoa sare mbili na kupoteza tatu, jambo linaloashiria kuwa pambano la leo litakuwa la upinzani mkali na la kujivunia.

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kuona kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia leo Oktoba 8, 2025, kikionesha uwezo, nidhamu, na ari ya ushindi ili kuhitimisha kampeni zao kwa heshima na matumaini ya mafanikio makubwa siku zijazo.

Matokeo Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

🔴 Matokeo Timu ya Tanzania vs Zambia na Taarifa za Mchezo Mubashara (Live Updates)

Matokeo ya Muda Halisi:

Tanzania 🇹🇿 [0] – [0] 🇿🇲 Zambia

Angalia Hapa >> Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  2. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  3. Tanzania vs Zambia Leo Oktoba 8 2025 Saa Ngapi?
  4. FIFA Yairuhusu Fountain Gate Kufanya Usajili Nje ya Dirisha la Usajili
  5. FIFA Yamteua Eng. Hersi Said Kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya Wanaume Duniani
  6. Djigui Diarra Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba 2025/2026
  7. Ahmad Ali Ashinda Tuzo ya Kocha Bora Mwezi Septemba 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo