Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025

Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025 | Matokeo ya yanga leo dhidi ya Wiliete Sc

Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025

Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025Hatimaye pazia la michuano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu barani Afrika linafunguliwa rasmi leo Ijumaa, Septemba 19, 2025. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, watashuka dimbani kuwakabili wenyeji wao Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hii ndiyo safari mpya ya Yanga katika kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye mashindano makubwa ya klabu barani Afrika, ikiwa na malengo makubwa ya kufika hatua ya makundi kwa mara ya tatu mfululizo. Mchezo huu wa Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025 utapigwa katika dimba la 11 de Novembro lililopo Talatona jijini Luanda, Angola, lenye uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 48,500. Saa 12:00 jioni kwa saa za Tanzania, macho yote yatakuwa yakielekezwa Angola, ambapo Yanga inataka kuanza vyema kampeni zake.

Baada ya kutoka kwenye Dabi ya Kariakoo na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika Ngao ya Jamii, Yanga iliingia kambini kujiandaa kwa safari ya kimataifa. Kikosi kiliondoka Dar es Salaam Jumatano usiku kupitia Ethiopia na kutua Angola mchana wa siku hiyo. Timu ilipata muda wa kupumzika kabla ya kufanya programu mbili za maandalizi, ikiwemo mazoezi ya mwisho katika uwanja wa mechi na kupitia video za wapinzani wao.

Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025

Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025

Wiliete Sc VS Yanga Sc

Kauli ya Uongozi wa Yanga

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine, alisisitiza kuwa Wiliete siyo timu ya kubezwa:

“Wapinzani wetu ni mabingwa wa Angola, huwezi kuwa bingwa kwa bahati mbaya. Tumefanya tathmini ya kina juu ya kikosi chao na tunapaswa kupambana kufikia malengo yetu. Niwaombe mashabiki watuombee dua njema na naamini tutapata matokeo mazuri.”

Wachezaji wa Hatari wa Wiliete SC

Katika kikosi cha Wiliete, kuna majina matatu yanayotazamwa kwa makini kutokana na uwezo wao:

  • Agostinho Calunga (Kipa)
  • Beni Jetour (Kiungo)
  • João Chingando Manha ‘Kaporal’ (Mshambuliaji)

Kaporal ndiye mchezaji hatari zaidi baada ya kuonyesha ubora katika CHAN 2024, akifunga mabao mawili dhidi ya Zambia. Safu ya ulinzi ya Yanga italazimika kuwa makini zaidi na mshambuliaji huyu.

Malengo ya Yanga Msimu Huu

Baada ya kufika hatua ya makundi kwa misimu miwili mfululizo, safari hii Yanga ipo chini ya kocha mpya Romain Folz, raia wa Ufaransa. Malengo makuu ya klabu ni kuhakikisha inafuzu tena hatua ya makundi na kuendelea kujenga historia ya soka la Tanzania barani Afrika.

Rais wa Yanga, Hersi Said, alipokuwa akifunga dirisha la usajili alisisitiza:

“Usajili wa msimu huu ni bora zaidi ya miaka ya nyuma. Pamoja na mafanikio ya ndani, bado tuna deni kwa mashabiki wetu – kuhakikisha tunafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa. Tunataka kufika hatua kubwa zaidi ya makundi.”

Rekodi ya Yanga Dhidi ya Timu za Angola

Historia inaonyesha Yanga imekuwa na matokeo mazuri dhidi ya timu za Angola kwenye michuano ya CAF:

  • 2007 vs Petro de Luanda (Ligi ya Mabingwa Afrika): Yanga ilipoteza 2-0 ugenini lakini ikashinda 3-0 nyumbani na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2.
  • 2016 vs G.D. Sagrada Esperança (Kombe la Shirikisho): Yanga ilishinda 2-0 nyumbani na kupoteza 1-0 ugenini, ikasonga mbele kwa jumla ya 2-1.

Rekodi hii ni dalili kwamba Yanga inaweza kupata matokeo mazuri dhidi ya Wiliete endapo itaonesha nidhamu na ubora mkubwa uwanjani.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za CAF Leo 19 September 2025
  2. Gamondi Atamba na Singida BS Baada ya Kutwaa Ubingwa wa Haraka
  3. Ratiba ya Mechi za Leo 18 September 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo