Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii 08/08/2024

Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii 08/08/2024 | Matokeo ya Azam fc Dhidi ya Coastal Union Leo

Klabu ya Azam Fc leo itakutana na Coastal Union katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Ngao ya jamii ambao umepangwa kuchezeka katika uwanja wa Amaan, Zanzibar leo saa 10 jioni.

Mchezo huu unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa kutokana na maandalizi ambao pande zote mbili wamefanya katika kipindi hichi ambapo vilabu hivi vilikua katika kambi maalumu za kujiandaa na msimu mpya.

Timu zote mbili zimekuwa katika maandalizi maalumu kwa muda sasa, zikijipanga kuhakikisha zinaanza msimu mpya kwa nguvu. Azam FC na Coastal Union, zote zimeweka kambi na kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha kuwa zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa tayari kwa ushindani. Timu hizi zimekutana mara kadhaa katika michezo ya kirafiki na ya mashindano, na kila mara zimekuwa zikitoa ushindani mkubwa, jambo linalotarajiwa pia kutokea leo.

Kila timu ina wachezaji nyota ambao huenda wakawa na uamuzi mkubwa katika matokeo ya mchezo huu. Coastal Union inamtegemea kipa Ley Matampi, aliyeshinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, pamoja na kiungo Charles Semfuko na mawinga hatari Hassan Abdallah na Denis Madzaka.

Azam FC, kwa upande wao, wanamtegemea mshambuliaji wao mpya Jhonier Blanco, ambaye ameonyesha makali yake katika mechi za kujipima nguvu. Viungo Feisal Salum na Jibril Sillah, ambao walikuwa na msimu mzuri uliopita, pia watakuwa muhimu katika kuunda nafasi za mabao. Kipa Mohamed Mustafa, aliyesajiliwa hivi karibuni, anatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Azam FC.

Makocha wa pande zote mbili wamekiri ugumu wa mchezo huu. David Ouma wa Coastal Union amesema kuwa wanajipanga kukabiliana na Azam FC kama timu, huku Bruno Ferry wa Azam FC akisisitiza umuhimu wa kupata ushindi ili kuingia fainali.

Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii 08/08/2024

Azam Fc5-2Coastal Union
  • GOAAAAAL! 14′ Azam FC 1-0 Coastal Union ⚽️ Sillah
  • 33′ Azam FC 1-1 Coastal Union
  • 🚨 M A T C H D A Y 🚨
  • Azam Fc 🆚 Coastal Union
  • 🏆 Community Shield 2024
  • ®️ Semi Final
  • 🏟 New Amaan Complex
  • 🕰 4.00 PM (E.A.T)

Angalia Hapa Kikosi Cha Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii 08/08/2024

Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii 08/08/2024

Mshindi wa mchezo huu atakutana na mshindi kati ya Yanga na Simba katika fainali ya Ngao ya Jamii. Matokeo ya mchezo huu pia yatakuwa na athari kubwa katika morali ya timu kuelekea msimu mpya wa ligi.

Historia ya Mkutano wa Timu Hizi

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (la CRDB) ambapo Azam FC iliibuka na ushindi. Coastal Union, chini ya kocha David Ouma, wameweka malengo ya kulipiza kisasi katika mchezo huu wa Ngao ya Jamii. Ouma amesisitiza kuwa wataingia uwanjani kama timu na sio kutegemea mchezaji mmoja pekee, akiamini kuwa ni njia bora ya kukabiliana na Azam FC.

Kwa upande wa Azam FC, kocha Bruno Ferry anaamini kuwa mechi hii haitokuwa rahisi, lakini wanajipanga kuhakikisha wanapata ushindi ili kuingia fainali na kutwaa taji la Ngao ya Jamii.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024
  2. Nchi za Afrika Zilizopata Medali za Olympics 2024
  3. Vituo vya Kukata Tiketi Mechi ya Ngao ya Jamii Yanga vs Simba
  4. Matokeo ya Ngao ya Jamii 2024
  5. Washindi wa Ngao ya Jamii Miaka Yote
  6. Rekodi za Simba na Yanga Kufungana
  7. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo